Bakari China
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 254
- 588
Habari wakuu wa JF! Hapa ni Mchina Bakari, ni muda mrefu hatujaonana.
Leo nitawafundisha namna ya kupika chakula kizuri cha Kichina, jina lake ni 番茄炒蛋, ambalo linamaanisha nyanya na mayai.
Kabla ya kupika, unatakiwa kuandaa vyema kwa mapishi yako. Malighafi yanapatikana sokoni, nyanya moja na mayai mawili tu.
1. Ikate nyanya kipandekipande. Ukubwa wa kila kipande usijali, kama upendavyo tu.
2. Weka mayai kwenye bakuli dogo, tia chumvi na ukavuruga kwa vijiti vya kulia (chopsticks). Unaweza kuvinunua katika supamakiti.
3. Washa jiko lako, halafu weka mafuta kwenye sufuria. Utakapoona moshi ya mafuta ndipo utaweka maji ya mayai kwenye sufuria. Lazima ukumbuke kuvuruga mara kwa mara ama sivyo mayai yataunguza.
4. Tia vipande vya nyanya halafu uvivuruge pamoja na mayai. Baada ya sekond 30 hivi chakula kitamu tayari!
(Katika hatua ya namba 4, kama ukipenda unaweza kutia ketchup(mchuzi wa nyanya), lakini Wachina wengi hawafanyi hivyo)
Sasa chakula tayari, unaweza kukila pamoja na wali(kama Wachina wanavyofanya) au ugali.
Jaribu kupika mwenyewe! Usiende mgahawa wa Kichina bali jipikie mara ijayo!