Nyanya ya F1 yenye matunda makubwa kama ya Tengeru 97

Nyanya ya F1 yenye matunda makubwa kama ya Tengeru 97

Gomegwa G

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
414
Reaction score
539
Habari za saa hizi wadau.

Naomba msaada juu ya swala hilo tafadhali. Naomba kama kuna mdau unajua nyanya yoyote chotara F1yenye matunda makubwa na yenye umbo la mviringo dizain ya Tengeru 97 anisaidie.

Nimekutana na nyanya kama Eden F1 na Asila F1 ambazo nimeambiwa hazina ishu huku napoishi. Huku nyanya iloyochongoka haina ishu kabisa.

Msaada wadau.
 
Picha tafadhari na sie tufaidike..
Ni kama hizi hapa kwenue picha.
Hizi ni ndogo tu nilizozikuta lakin zinakuwa kubwa zaid ya hapa
20200829_164753.jpeg
20200829_164733.jpeg
 
Mkuu cheki na nyanya Nyota F1 au Milele F1 View attachment 1552230
Shukrani sana mkuu. Hii naona ni yenyewe kabisa. Ntaifuatilia nione.
Lakin vipi mkuu una experience na hii nyanya ya TO 135 F1?
hii naambiwa ni nzuri na wengine wananitia wasiwasi kuwa ipo kama zile nyingine za kuchongoka
 
Hizi ndio Nyanya nilizozifahamu tangu ninakuwa, hizi mchongoko nadhani Wengine huziita Nyanya Mshumaa nimeziona kuanzia miaka ya mwishoni wa 90 au mwanzoni wa 2000 kama sikosei.
Kwa hiyo mkuu. Hizi nyanya za milele na nyota hazichongoki na siyo ndogo sana?
 
Kwahiyo mkuu. Hizi nyanya za milele na nyota hazichongoki na siyo ndogo sana?
Mimi sio Mtaalamu Mkuu nilikuwa tu nazielezea hizo Nyanya za mviringo nilizozifahamu tangu zamani na ningetamani ziendelee kuwepo....maana sasa hivi hizi mchongoko ndio zimejaa sokoni.
 
Mimi sio Mtaalamu Mkuu nilikuwa tu nazielezea hizo Nyanya za mviringo nilizozifahamu tangu zamani na ningetamani ziendelee kuwepo....maana sasa hivi hizi mchongoko ndio zimejaa sokoni.
Sawa mkuu. Ntazifuatilia hizo
 
Kwahiyo mkuu. Hizi nyanya za milele na nyota hazichongoki na siyo ndogo sana?
Mimi binafsi nazilima hizo hazichongoki na zinakua kubwa mno wastani wa nyanya kubwa 90 zinajaza ndoo ya Lita 20 mfuto
 
Mkuu inategemea na unapolima, ila tumia F kipato hii huvumilia hata hali za hewa, na hazina tabia ya kunyauka ovyo
 
Vipi Rio glande,umeshawahi ijaribu???,Maana niliwahi kulima Wauzaji wa Sokoni waliipenda sana walikuwa wanavutiwa na rangi nyekundu iliyoiva
 
Vipi Rio glande,umeshawahi ijaribu???,Maana niliwahi kulima Wauzaji wa Sokoni waliipenda sana walikuwa wanavutiwa na rangi nyekundu iliyoiva
Sidhan kama Rio glande ni nyanya chotara. Sijaipanda lakin nimeiona kwa dogo mmoja aliinunua juzi. Nayo ina matunda ya kuchongoka.
 
Back
Top Bottom