Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Vipimo
Nyanya za mshumaa/chungu 20 kiasi
Kitunguu 1
Nyanya/tungule 2
Mafuta ya zaytuni (olive oil) 3 vijiko vya supu
Pilipili mbichi 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) 3 chembe
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha nyanya za mshumaa/chungu kisha zichemshe kidogo.
- Mwaga maji, menya maganda na ukatekate vipande vipande.
- Katakata kitunguu, nyanya vipande vidogovidogo (chopped)
- Saga au katakata pilipili mbichi na thomu.
- Weka mafuta katika sufuria, tia vitu vyote pamoja. Kaanga kwa muda huku unakoroga hadi iwive.
- Pakuwa katika chombo, nyunyizia mafuta ya zaytuni.