Kesho nakutana na DPP kuweza kuongea naye juu ya ushahidi niliowasilisha juu ya walioiba fedha za umma kupitia Kagoda
Nina picha, video zinazoonyesha wizi wa Kagoda wazi.
Kinara wa wizi huu ni Rostam Aziz aliyekuwa mbunge wa Igunga.
Wa pili ni Yusufu Manji
Wanaohusika serikali inadai haiwafahamu. Nawafahamu na wanakaa Kinondoni na walifanya hivyo kwa maelekezo ya Rostam Aziz.
Walioenda Brela kusajili kampuni tuna picha zao na majina yaliyoandikwa ni ya uwongo.
Jina Kagoda linatokana na KATO na GODA.
Angalia nyaraka zilizoambatanishwa.
Baada ya Kagoda kufunguliwa, ilitakiwa itengenezwe account ambayo ilitengenezwa CRDB na mdhamini alikuwa Yusufu Manji (angalia attachment chini ya 1st post ikionyesha na account number).
BoT wanawajua wahusika wote kwani pesa zilihamishwa kwa ushirikiano na CRDB.
Bharat Goda kwa maelekezo ya Rostam Aziz alipeleka barua inayoonyesha kuwa Bil 8 ziende kwenye account tofauti. Viambatanisho vipo, hivyo zikaongezwa kwenye Bil 25 nyingine iliyokuwa kwenye account tofauti.
Bil 33 baadae zilihamishwa kwenda kwenye account nyingine ambayo Yusufu Manji aliidhamini huko Holland Branch
Pesa hizi baadae zilitoroshwa kwenda Dubai kwa ushirikiano wa Yusufu Manji kwenye mafungu ya $ milioni moja moja. Kwa kutumia kampuni ya Quality Finance Corp