Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
Nyaraka muhimu za ofisi ya mwanasheria mkuu zaibwa
Na Ramadhan Semtawa
GARI aina ya Toyota Hiace (Custom), ikiwa na nyaraka muhimu za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, imeibwa katika yadi ya maegesho ya magari ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tabata.
Kuibwa nyaraka hizo, ambazo zilikuwa zikienda ofisi ya kanda kwa ajili ya kuendeshea mashtaka, kumekuja wakati serikali ikiwa katika mchakato wa kufungua ofisi mbalimbali za kanda kutekeleza Sheria ya Kuendesha Mashitaka ya mwaka 2008.
Duru za habari za kuaminika ambazo zilithibitishwa kwa kifupi na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, zinasema tayari watu zaidi ya watatu wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio hilo.
Kamanda Kova, ambaye aliahidi kulizungumza suala hilo kwa kirefu leo, alisema: "Ni kweli hilo tukio lipo, lakini tayari kuna watu wamekwishakamatwa na wanahojiwa... taarifa kamili nitaitoa kesho (leo)."
Alipoulizwa kuhusu idadi hiyo ya watu zaidi ya watatu, alijibu: "Kama nilivyokwambia brother (kaka), si unajua hapa Dar lazima kila kitu kinatakiwa kiende kwa uhakika zaidi.
"Mimi sikujua kama utaniuliza leo, kwa hiyo sikuwa nimeandaa hizo taarifa, lakini kesho (leo) nitazungumza wakati vyombo vyote vikiwepo."
Kova alipoulizwa zaidi kama tayari gari hilo na baadhi ya nyaraka na vitendeakazi kama kompyuta vimekwishapatikana, alisisitiza: "Njoo ofisini kesho."
Wakati Kova akisema hayo, duru hizo za habari za Mwananchi, zilidokeza kwamba gari hilo lilibwa katika mazingira tata ndani ya yadi.
Kwa mujibu wa duru hizo, gari hilo ni jipya na ni sehemu ya magari zaidi ya sita ambayo yamenunuliwa rasmi kwa ajili ya kusambazwa kwenye ofisi mpya za kanda kwa ajili ya kazi za kuendesha mashitaka.
Duru hizo zilifafanua kwamba gari hilo lilikuwa na kompyuta na nyaraka nyingine za ofisi tayari kupelekwa katika kanda.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), imekuwa katika mchakato wa utekelezaji wa Sheria Mpya ya Kuendesha Mashitaka ya mwaka 2008 kwa kufungua ofisi za kanda kwa ajili ya kuendesha mashtaka. Awali, Jeshi la Polisi ndilo lililokuwa likiendesha kesi.
Lakini sheria hiyo imetenganisha mamlaka ya kuendesha mashitaka kutoka mikononi mwa polisi.
Tayari mpango huo awali ulianza kama majaribio katika baadhi ya mikoa kama Tanga, Arusha, Mbeya na Mwanza, huku DPP Feleshi akisema hadi sasa tayari mpango huo umeanza rasmi karibu katika kila makao makuu ya mkoa.
huu ni uzembe wa hali ya juu kwa upande wa AG's offices haiwezekani kabisa