Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NYARAKA ZA SYKES ZINAVYOELEZA HARAKATI ZA KUDAI UHURU NA HISTORIA YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Naomba ruhusa nianze na historia ya babu yangu.
Footnote No. 10 inaeleza historia ya babu yangu Salum Abdallah alivyooongoza mgomo wa nchi nzima wa mwaka 1947 ulioanza na mgomo wa wafanyakazi wa reli Tabora.
Huu ndiyo ulikuwa mwaka babu yangu alipohamia Tabora kwa uhamisho wa karakana kuu ya reli ilipotolewa Dar-es-Salaam na kupelekwa Tabora.
Babu yangu aliuza nyumba yake Mtaa wa Mbaruku na hakurudi tena Dar-es-Salaam.
Nyumba hii ilikuwa jirani na nyumba ya Aziz Ali kabla Aziz Ali hajahamia Mtoni alikojenga nyumba ya fahari ya vigae na vioo.
Wakati ule hakuna Mwafrika aliyekuwa na nyumba kama ile.
Salum Abdallah alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU Tabora 1954 na Tanganyika Railways African Union (TRAU) 1955.
Aliongoza mgomo wa railway wa 1949 na mgomo wa 1960.
Sasa tutazame hizi Nyaraka za Sykes katika "In Praise of Ancestors," makala iliyozua taharuki.
Katika rejea kutoka Nyaraka za Sykes foot note no. 16 kuna barua ya Julius Nyerere ya tarehe 10 August, 1953 anamwandikia Gavana Edward Twining.
Kwa mara yangu ya kwanza kuiona saini ya Mwalimu Nyerere nje ya saini yake kwenye noti nimeiona kwenye hizi Nyaraka za Sykes.
Lakini nilikuwa nasisimkwa na mwili pamoja na akili pale Ally Sykes alipokuwa akinieleza mazingira yaliyopelekea kuandikwa kwa barua fulani.
Kitendawili nilichokutananacho kilikuwa rasimu ya katiba ya TANU.
Katiba hii iliyeyuka kama moshi.
Haipo kwenye Nyaraka za Sykes wala Maktaba ya CCM Dodoma.
Katika Maktaba ya CCM nilionyeshwa majalada mengi lakini karibuni yote kulikuwa na nyaraka zilizonyofolewa.
Nilibahatika kuliona jalada la Hamza Mwapachu na jalada la Abdul Sykes.
Majalada yote haya hayakuwa na hata karatasi moja ndani.
Nilipata tabu sana na mhariri wangu wa kitabu cha Abdul Sykes alipokuwa anaupitia mswada kwa ajili ya kuchapa kitabu.
Mimi nilikuwa nimeandika nyaraka zimeibiwa yeye akinitahadharisha kuhusu neno hilo la kuibiwa akiniambia linaweza kusababisha matatizo tukashitakiwa.