Nyashinski ataka kulipwa 20m kwenye interview, Wakenya wamjia juu

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,043
Ni kweli Nyashinski ameanza kulewa umaarufu? Hiko ndio kitu kinachoonekana kwa msanii huyo kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki wa nchini Kenya.



Tuhuma hizo zimeibuka kupitia gazeti maarufu nchini Kenya baada ya msanii huyo kudaiwa kutaka kulipwa kiasi cha shilingi milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na milioni 20 za Kitanzania kautika kila interview atakayoalikwa.

“Alisema anataka tumlipe ndio aje kwenye show. Asipochunga ata-fade haraka. Nasikia amekuwa akiifanya hata studio fulani hivyo. Kwani yeye ni nani?,” limeandika gazeti hilo wakati wakimnukuu mmoja ya waaandishi ambao walikataliwa na Nyashinski kufanya mahojiano.



Nyashinski amedaiwa kuwa alikataa kufanya mahojiano hayo na kipindi kikubwa nchini humo cha runinga ambacho kinaruka kila siku za Ijumaa usiku.

Wakati huo huo Bongo5 imemtafuta mmoja ya waandishi kutoka nchini humo amethibitisha kuwa hiyo ndio tabia mpya ya msanii huyo na ameanza kuwavimbia mpaka wasanii wenzake kwa kuwakatalia kufanya nao kolabo.

Source: Bongo5
 
Mbona hio jina ndio nalisikia leo!
 
Ndo nani huyo, hebu weka picha ake tumuone.

Aroo, Kama mziki ndo rahisi ivo na Mimi kesho natafuta umaarufu.
 
Huyu si ndo Kusaga alisema alikuwa anaomba kufanya show ya Fiesta hata bure?
 
Kitaa kuna demu anaitwa Nyanshiki, naona yeye kaongeza madoido kiduchu.
 
She has her own money, and a lot of it. Doesn't
anyone know who she is?! Seriously people, stop it.
She isn't a gold digger. They've been married for a
decade. She co-founded Marchesa 3 years BEFORE she even married him.
 
She has her own money, and a lot of it. Doesn't
anyone know who she is?! Seriously people, stop it.
She isn't a gold digger. They've been married for a
decade. She co-founded Marchesa 3 years BEFORE she even married him.
We nae unakopigi comments huko unaleta hapa. Ulicho paste leo umeingia cha kike...nini hiki sa
 
Mtoa mada ungemalizia tu ksh 1mil = 21,688,000/= tsh.
Nilikuwa sijui!!sasa tz na kenya kwa utofauti huo mkubwa tutafanya biashara gani za pamoja?kweli tunamuhitaji Mungu ili atusaidie sana maana tunaweza tukawa tunakurupuka halafu tunajihisi tunawaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…