maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,311
- 15,640
Kweli sijui kama TTCL wanajielewa aisee. Unapopita maeneo mengi yenye mazingira mazuri na yaliyopendeza, unakutana na nyaya za TTCL zilizopita hovyohovyo, nyingine zikiwa zinaning'inia chini, huku nguzo zimepinda ovyo bila anayejali. NEMC wanapaswa kuwadhibiti hawa jamaa, maana inaonekana hawajui au hawajali kabisa.
Kiufupi, taswira ya jiji la Dar es Salaam inachafuliwa na hizi nyaya za TTCL. Zimekuwa kama uchafu; hazina mpangilio, utadhani zimefungwa na mateja. Sio Oysterbay, Masaki, Posta, Mikocheni wala Mbezi – kote ni uchafu wao unaoharibu sura ya mji.
TTCL, hebu kuweni serious basi. Zifungeni kwa mpangilio, zipitisheni chini, au mkate na kuziondoa kabisa kama hazitumiki.