Nyenzo yetu, Kesho yetu!

Nyenzo yetu, Kesho yetu!

Akida MALCOLM X

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
492
Reaction score
456
"Education is the passport to the future,for tommorow belongs to those who prepare for it today-Malcolm X!" Kila nikiangalia mwenendo wa sekta yetu ya Elimu naikumbuka kauli husika!

Ni suala lililo wazi,hakuna nyumbani zaidi ya Tanzania. Hili ni jahazi letu ingawa wahuni wachache wanaishi wakifikiri ni lao! Kichekesho!

Elimu ya Tanzania ipo kwa masrahi ya kisiasa, ndo maana hua najiuliza Mkapa alitumia kigezo gani kuliunganisha somo la physics na chemistry!

Ambapo ukiangalia hata definition zake tu, hazina mfanano wowote! Moja limejikita kwenye nishati lingine hali katika maada! Acha kichekesho hicho,leo matokeo tunatoa kupitia gpa!

Ni upuuzi mtupu kuzani kwamba tutaboresha elimu bila kumboresha Mwalimu! Kwa miaka yote serikali ya CCM,inachofanya ni kuongeza takwimu tu,ila sio ubora! Politics! Zinaitafuna nchi hii!

Kutokuona kitu kinacho onekana ni balaa,lakini kuona kitu wakati hakipo ni majanga! Walimu wamekosa morali wa kazi! Wanaojiriwa leo tayari walisha choka kufanya kazi,wanachofanya ni kulinda ajira tu! Na ukitaka ng'ombe atoe maziwa,mkumbuke mkata nyasi.

Leo walimu wanaishi kwa matumaini mithiri ya wagonjwa wa UKIMWI! Likizo shida,mishahara midogo, madaraja hayapandishwi,ila ESCROW/EPA/RICHMUND hela zinapigwa kiDOWANS! Sisi ni taifa pekee lenye pesa za kuiba ila sio kwa ajili ya huduma kwa watu wake.

Huku kwetu kuna mradi wa WEKEZA chini ya ufadhili wa US, kichekesho wamekuja na format mpya ya scheme of work! Wanatuibia dhahabu kesho wanakuja na misaada ya kipuuzi! Manju wa Bagamoyo hashangai,maana kuomba ni sehemu ya ilani ya chama chao,nonsense.

Knowledge is power,tutaendelea kua manamba kwenye ardhi yetu,watumwa kwenye viwanda vyetu,na misukule kwenye vitega uchumi vyetu,tunaendelea ndani ya umasikini,ila haki,usawa na uhuru,sio hisani! Elimu ndo nyenzo yetu!
 
Back
Top Bottom