Nyerere alipo fariki aliondoka na maadali ya uongozi na Makweta aliondoka na Elimu

Qualifier

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
1,252
Reaction score
405
Ndugu wana Jf ninaandika makala hii kwa uchungu na masikitiko makubwa, wakati wa utawala wa mwalimu Nyerere viongozi walikuwa wadilifu na walionyesha uzalendo wa hali ya juu. kila kiongozi aliye chaguliwa na wananchi na hata aliye teuliwa na Mamlaka yoyote ile alifanya kazi kwa maslahi ya Tanzania, tofauti na sasa kila kiongozi awe amechaguliwa na wananchi au kuteuliwa kazi ya kwanza ni kujali maslahi yake binafsi. Sasa kwa upande wa Elimu kuna upungufu mkubwa saana wa walimu wa masomo ya Sayansi na hisabati katika shule zetu za sekondari, waziri wa Elimu haoni kama kuna tatizo lolote, hivi Tanzania baada ya miaka kumi kuanzia sasa itapata wapi wataalamu wanao tokana na masomo ya sayansi pamoja na hesabu? mbona hatuoni jitihada za maksudi za kuliondoa au japo kupunguza tatizo hili? ninacho kumbuka mimi enzi za waziri Makweta walimu wa masomo ya sayansi na hesabu walikuwa wanalipwa mishahara tofauti na walimu wa masomo ya art, na hata posho ya kufundishia ilikuwa tofauti kati ya walimu wanao fundisha masomo ya sayansi na ya art. Hii ilifanya wanafumzi wengi wapende kusoma masomo ya Sayansi na ndio hawa walimu wachache sana waliopo sasa ambao umri wao sasa wengi wanaelekea kustaafu hapo ndipo utakapo kuwa mwisho wa kufundisha masomo ya sayansi na hesabu katika shule zetu, hivi wazir wa Elimu haoni kuwa hili ni tatizo? wakati nchi zingine zinakimbia kuelekea katika ulimwengu wa sayansi na tekinolojia, sisi tuna chapa usingizi hivi tutakuwa wageni wa nani? bado tumekumbatia sera ambazo baada ya muda zitaliangamiza taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…