Nyerere Day iadhimishwe bara zima la Afrika kumuenzi Baba wa Afrika

Nyerere Day iadhimishwe bara zima la Afrika kumuenzi Baba wa Afrika

King Jim

Member
Joined
Aug 12, 2024
Posts
6
Reaction score
16
Tarehe 28 September 1999 redio SAFM (South Africa) ilitangaza kifo cha Mwl Nyerere.

20241013_095408.jpg
Tena wakarudia kutangaza 11 October 1999 kuwa Mwl ametutoka huko Uingereza, Tena wakatangaza 14/10-1999.
20241013_095405.png
Baada ya kila tangazo waliomba radhi kwa taarifa zisizosahihi lakini kinachoshangaza ni kwanini redio ya Ughaibuni ijitese sana kisa kifo cha raisi masikini mpaka kukosea mara kadhaa kwa kutoa taarifa za masikitiko?

Ni wazi mchango wa Mwl, hauwezi kufichika kamwe ndio maana hata SABC (Kituo cha Televisheni huko Kwa Madiba) kilirusha LIVE mazishi ya mwalimu. kutoka mashariki mwa Afrika.

Mwl Nyerere ni BABA WA AFRIKA. Japo wengi tumemzoea kama Baba wa Taifa. Pasipo na Nyerere, Afrika yetu hii ingebeba sura mpya sana na sikama tuliyonayo leo hii.
20241013_095623.jpg
Ukiacha madini, ardhi, maziwa, mito milima na mbuga za wanyama, zawadi au baraka nyingine tuliyopewa na Mungu kama upendeleo ni kuwa na kiongozi kama Mwalimu Nyerere.

Ni miaka mingi sana tunamkosea heshima mzee lakini ni wakati sasa umefika, Afrika imlipe hata kwa kulienzi jina lake tu maana mchango wa fikra zake zimeinufaisha Afrika yote kwa ujumla.

"Mwalimu Nyerere, Baba wa Afrika"

Akiwa na umri wa miaka 77, miezi sita na siku moja zaidi, tarehe kama ya kesho mwaka 1999 Mwalimu alivuta pumzi yake ya mwisho huko Uingereza baada ya kupambana sana na cancer ya damu (Leukemia). "Baba wa Afrika" akatutoka.

Safari yake iliyosababisha mimi leo kumpa jina la "BABA WA AFRIKA" rasmi ilianzia March-1955 baada ya Mwl kufanya uamuzi wenye busara wa kuacha kazi yake ya ualimu iliyokuwa ikimlipa na kuchagua kufanya siasa kwa barua hiyo hapo chini kwa father aliyekuwa mkuu wake.
20241013_095419.jpg

Kwakukosa kazi alirudi kijijini kwao mpaka hapo alipofatwa na Mh.Kambona arudi Dar kukiendesha chama chao kipya cha TANU kwani fikra zake zilikuwa wazi kuwa hakukuwa na wakumkaribia.

Ndipo ukombozi wa Afrika ukabeba sura mpya duniani kote, ni sura ya Nyerere.

1958, Mwl aliongoza kikao mjini Mwanza kilichoanzisha PAFMECA ambayo ndio shirika lililomfanya Mandela leo aitwe Madiba na kumleta duniani kutoka kwenye ardhi ya ubaguzi.

Mwalimu alipinga vikali ubaguzi uliofanywa kwa kina Madiba, na miezi michache kabla Tanganyika haijapata uhuru, Mwl alitaka Afrika Kusini 🇿🇦 itolewe kwenye jumuiya ya Madola na kama si hivyo Tanganyika haitajiunga kwenye jumuiya hiyo, mkutano uliisha kwa S.A ya mkaburu kujitoa yenyewe kwa kuona aibu.

Mwaka 1965,Mwl alianzisha hoja ya nchi za kiafrika kujitoa kwenye umoja wa madola baada ya bwana Ian Smith kupewa uhuru bandia huko Zimbabwe 🇿🇼. Na mbio hizo zikasababisha Southern Rhodesia kufukuzwa jumuiya ya madola kama njia moja ya kinafiki ya kukubaliana na mwalimu na kuepusha mgawanyiko mkubwa usiohitajika.

Hivyo haikuwa bahati mbaya kwa Che Guevara kutumia Tanzania 🇹🇿 kwa maandalizi yake kabla hajajiunga nchini Congo 🇨🇩 kwa mapambano ya ukombozi. Kwani aliingia na kutoka Congo 🇨🇩 kupitia Tanzania.
20241013_095515.jpg
Hakuna nchi ambayo haikufaidika na msaada wa Mwalimu katika kujikomboa kwao kwani;
20241013_095529.jpg
FRELIMO ya Msumbiji 🇲🇿 ilianzishwa Tanzania 🇹🇿,
APC ya kina Mandela ilifungua tawi lake la kwanza Tanzania baada ya kufungiwa huko Bondeni.
Bado nchi zingine zilifika Tanzania kama nyumbani kipindi wanadai uhuru wao,
UNIP ya Zambia 🇿🇲,
The Malawi Congress Party 🇲🇼,
ANC & PAC za Bondeni 🇿🇦,
MPLA of Angola 🇦🇴,
SWAPO of Namibia 🇳🇦,
ZANU & ZAPU vya Zimbabwe 🇿🇼,
Na wapiganaji wengine kutoka mbali kama huko Comoros 🇰🇲 walikaa na kusikiliza Lecture za mwalimu kuhusu ukombozi.
20241013_095535.jpg
Mwalimu ndiye aliyemtengenezea pasipoti ya kusafiria Mandela na kumpa maneno ya kusema huko kwa mfalme wa Ethiopia 🇪🇹 Emperor Haile Selassie alipokuwa anatoka Dar kwenda kuzurula duniani baada ya kuruhusiwa na chama chake cha ANC kwenda kujifunza ili waanze kutumia njia zingine kudai uhuru.

Bado kuwa rais wa watu ndiko kulimwacha Mandela mdomo wazi baada ya kufika nyumbani kwa Nyerere na kukuta haishi maisha ya kifahari wala hatumii gari la kifahari namaanisha kama hii Landlover party ingefanyika muda huo, mwalimu angeikosa kabisa hii ilikuwa mwaka 1962 baada ya Nelson Mandela kutoroka South Africa na kutaka kuhudhuria kikao cha PAFMECA huko Addis Ababa kwa kuomba msaada wa uhuru wa watu weusi huko Bondeni.
20241013_095433.jpg
Mwalimu hajawahi uchekea unyanyasaji wa watu ndio maana alifunga ubalozi wa Israel 🇮🇱 na kufungua wa Palestine 🇵🇸 baada ya kujua namna Israel ikisumbuana na Palestine, kisha akamchapa Iddi Amin wa Uganda 🇺🇬, na kuwafokea watu wa Umoja wa mataifa na masharti yao magumu kwa nchi za Africa (SAP's) kiufupi alijua nini anafanya.

Mwl hakuwahi ogopa vitisho vya wareno kwa kuzisaidia nchi kama Angola 🇦🇴 na Msumbiji 🇲🇿 hata waliporusha ndege kutoa matangazo ya vitisho huko Dar kumuonya Mwalimu juu ya ukubwa wa Wareno.
20241013_095509.jpg
Mwalimu alihusika sana kuwaonganisha kina Mugabe na wenzie waliokuwa wakidai uhuru kwa kutengana, mpaka leo Mugabe anajua fika mchango wa mwalimu na kama angelikuwepo nasi leo angeunga mkono hoja yangu hii ya leo ya kutaka Nyerere day iwe Public Holiday kwa bara zima la Afrika

Kuonesha hakuwa mnyonge wa kutetea hoja zake Mwl alishawahi gombana na Kwame Nkrumah wa Ghana 🇬🇭 aliyekitaka cheo chake cha Ubaba wa Africa kwa hoja za kibabe kwenye vikao vya OAU na Mwalimu akashinda kwa kuwashawishi wajumbe wengi zaidi japo pia kwenye kikao hicho kulikuwa na kukoseana heshima kama alivyosimulia Rais Mkapa ambaye kwenye kitabu cha maisha yake, amemuelezea zaidi Nyerere kuliko hata yeye mwenyewe, inashangaza sio?
20241013_095605.jpg
Alisimulia Jeanette Hartmann (mkufunzi wa UDSM) kuwa Mwl aliandika kwa mkono wake mwenyewe Azimio la Arusha ambalo liliifanya Tanzania kuwa nchi ya kijamaa na kuwatisha mabepari kote duniani.

Mwaka 2006 kanisa katoliki lilifanya uchunguzi wa maisha ya Mwl kutaka kumpa UTAKATIFU japo aliishia kuwa "Mwenye heri" ambayo ni hatua moja kabla hujawa MT.

Hakika "Zidumu fikra za Mwalimu Nyerere" na siku hii ikumbukwe Afrika kote kwani siku hii Baba wa Afrika alipumzika baada ya kusudi lake hapa duniani.
 
Baada ya JKN, ni JPM halafu BWM kwa hapa Tanganyika.

Mandela, amepata umaarufu kwakuwa ubaguzi na unyanyasaji kwa watu weusi uliendelea kwa kipindi kirefu zaidi(1994) hadi dunia ilipokuwa imechangamka na mawasiliano kuimarika duniani, kiasi cha kila mtu kujua yanayoendelea pale.

Zidumu fikra zangu!
 
Baada ya JKN, ni JPM halafu BWM kwa hapa Tanganyika.

Mandela, amepata umaarufu kwakuwa ubaguzi na unyanyasaji kwa watu weusi uliendelea kwa kipindi kirefu zaidi(1994) hadi dunia ilipokuwa imechangamka na mawasiliano kuimarika duniani, kiasi cha kila mtu kujua yanayoendelea pale.

Zidumu fikra zangu!
Nashangaa kuona kila ukitajwa ukombozi wa Africa, wanamuweka Mandela tu, na hakuwahi kufikia nusu ya u smart wa Mwalimu.
 
Shida Africa ya sasa ina wanasiasa wengi kuliko viongozi.
 
Back
Top Bottom