Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NYERERE DAY: MAKTABA INAVYOMUADHIMISHA BABA WA TAIFA
Leo ni Nyerere Day.
Leo ni siku ya mapumziko.
Taifa linamuadhimisha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Maktaba yangu ni kati ya maktaba tatu zilizosheheni historia ya Mwalimu Nyerere.
Maktaba ya kwanza ni ya Dr. Salim Ahmed Salim ya pili ni hii yangu na ya tatu ni ya Brig. General Hashim Mbita.
Haya yameandikwa katika kitabu cha maisha ya Julius Nyerere waandishi wakiwa Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Ng'waza Kamata.
Nimedamka na Maktaba.
Napitia makala zangu zenye historia ya mengi aliyopitia Mwalimu Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Historia hii haifahamiki.
Hii ni historia ngeni kwa wengi na haikuweko wala haikupata kufahamika.
Naangalia picha za Mwalimu na ni picha za zamani sana na waliokuwa katika picha hizo na wakati huo wote wametangulia mbele ya haki.
Natazama video na kusikiliza audio nilizozungumza historia ya Julius Nyerere.
Najiuliza kipi niweke ambacho kitaeleza historia ya Mwalimu kama inavyostahili kuelezwa?
Hii si kazi rahisi.
Hii ni kazi ngumu sana lakini lazima juu ya ugumu wake ifanywe.
Lazima Maktaba imuadhimishe Baba wa Taifa kwa neno la kuandika, kwa picha na kwa sauti.
Tufunge safari:
View: https://youtu.be/Y7pYlUi09Rw?si=F1y5EqUEyY6-RxIB
Huenda wengi watastaajabu kufahamu kuwa nimehariri kitabu cha Jim Bailey, "Tanzania The Story of Julius Nyerere," (1993).
Halikadhalika nimeshirikishwa katika kumweleza Mwalimu katika kitabu cha maisha yake.
View: https://youtu.be/cDXRaONNaCY?si=AuFlrY3n_oJR3y8P
Kwa mukhtasari nimependa kuweka hapa machache yaliyopo Maktaba kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1922 - 1999).