Nyerere hakukosea serikali mbili, kikwete kakosea serikali mbili.

Nyerere hakukosea serikali mbili, kikwete kakosea serikali mbili.

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
2,469
Reaction score
586
Nyerere alikuwa sawa kabisa maana alikuwa akipinga utanganyika na uzanzibar na kujali utanzania.ndio maana smz kawa na kwa ajili ya zanzibar tu na haitambuliki kimataifa. zanzibar ilikuwa ni sehemu ya muungano wala sio nchi.umuhimu wa serikali ile ni kudumisha utamaduni wa kuisaidia serikali ya muungano kutoa huduma.

Kikwete kaibadili katiba ya znz kuitaja kama znz ni nchi,kaipa wimbo wa taifa na bendera pamoja na kutambulika kikatiba kwa vikosi vya ulinzi vya jku na kmkm.Utawala wa kikwete umekuza uzanzibar ambao hata nyerere hakutaka ufike huko.sasa tanzania kumezaliwa taifa la wazanzibar wanaojiona bora kuliko wengine na kutaka kujitenga. serikali mbili hazitafaa.
 
Enzi ya Nyerere Zanzibar haikuwa nchi. Sasa kama inajitambulisha kama ni nchi na ina bendera na wimbo wake wa Taifa, kwanini nasisi tusirejeshe TANGANYIKA yetu. La hasha, wakubali kurejesha katiba ya awali na Zanzibar iwe Sovereign state kama awali. Hapo tutakubali kuwa na serikali ya Mapinduzi na ya MUUNGANO.
 
Naunga kiuno hoja!
Sasa tuna nchi mbili ndani ya nchi moja,
i wapi Tanganyika yetu??
 
Back
Top Bottom