CCM ya Nyerere (CCM-NY) sio ya Mwinyi (CCM-MW), Mkapa (CCM-MK) wala Kikwete (CCM-KI)! Ile ya Nyerere iliongozwa na Azimio la Arusha lililokuwa na Miiko ya Uongozi! Kwenye CCM-NY hakuna aliyethubutu kujilimbikizia mali isivyo halali! Mwenye mali hakuruhusiwa kugombea uongozi wa CCM-NY! CCM-MW ilifuta Azimio la Arusha, madirisha yasiyo na nyavu ya kiuchumi yalifunguliwa! Kwa hiyo upepo "mzuri" wa kiuchumi uliruhusiwa lakini kwa kuwa hakukuwa na nyavu pia mbu, vumbi, wadudu wa bidhaa feki na bei rahisi walimaliza kabisa viwanda vyetu ambavyo havijanyanyuka hadi leo! Mpaka sasa we are consuming what we don't produce and we are producing what we don't consume! CCM-MW ilimzaa CCM-MK ambaye iliendekeza mno wezi ambao walipewa jina "zuri" la wawekezaji! Ukiongea jambo baya juu ya mwekezaji unaonekana wewe sio mzalendo! Wizi huu ulizaa ufisadi! CCM-MK iliwalea mno mafisadi na ukiongea vibaya juu ya mafisadi unaambiwa wewe ni "mvivu wa kufikiri" au "una wivu wa kike!" CCM-KI inaendeshwa kisanii: hakuna mipango yoyote zaidi ya ile iliyokuwapo ya kuingia Ikulu! Baada ya kuingia hawajajua wafanye nini! Usanii unaendelea kila nyanja: kwenye mapambano dhidi ya ufisadi wengine wanatakiwa wapumzike, wakati baadhi wanashtakiwa! Wengine wanapewa muda wa kurudisha hela walizoiba, wengine wanafunguliwa mashtaka bila kupewa huo muda! CCM-KI ni nyepesi mno kuona matatizo lakini ni nzito mno kuchukua hatua, imejaa woga na kuoneana haya! CCM hii inaonekana haina central command, kila mtu ni msemaji! Migawanyiko, vijembe, matusi, kukashfiana ili kutafuta cheap popularity kila kona! Usipokuwa na vijisenti kwenye CCM-KI sahau kabisa kuchukua fomu ya kugombea uongozi, utaaibika! CCM-KI si Chama cha Wakulima na Wafanyakazi: Ni Chama Cha Wafanyabiashara! Ukiambiwa CCM ina wenyewe, they always mean what they say, and say what they mean!