TANZANIA: PRESIDENT NYERERE THANKS BRITAIN FOR ITS | Archive Footage | ITN Source
Siku ya Uhuru Nyerere alituma salamu kutoka mkutano wa hadhara uliofanyika Dar.
Hebu jaribuni ku google kwanza...
JokaKuu, habari ya Madaraka Nyerere ni ya kusimuliwa, ushahidi uliowekwa na mkuu Kiranga unajieleza dhahiri kuwa nyerere alisherehekea uhuru wa zimbabwe kwa kuhutubia mkutano wa hadhara jijini dar es salaam. Kama anaweza kutuwekea link ama picture atakuwa kafanya jambo jema.jogi, Mundu,
..kuna kipande cha habari toka blog ya Madaraka Nyerere ambacho kina-suggest kwamba Mwalimu alikuwepo Harare siku Zimbabwe inapewa uhuru. fuata link niliyoiweka hapa chini.
From Butiama and beyond...: Visitors to Butiama: Ayoub 'Rasta' Laizer
jogi,
..huenda Madaraka Nyerere amekosea.
..lakini wewe subiri tu hapa JF ni jungu kubwa utapata jibu la uhakika.
nakala:
Jasusi, Kudi Shauri
Siku ya uhuru wa Zimbabwe Mwalimu alikuwa Dar-es-Salaam. Tanzania siku hiyo ilisherehekea kwa kutangaza siku kuu na Mwalimu alihutubia kwenye sherehe hizo. Mwalimu alienda Zimbabwe baadaye akiwa mgeni wa kwanza rasmi wa serikali ya Zimbabwe baada ya uhuru. Lakini siku ya uhuru alikuwa Dar-es-Salaam. Kiranga you are right on the money.
Kama aliyasema hayo basi ni maneno ya kisiasa kutoka kwa mwanasiasa! hivyo hayana uzito wowote kwangu mimi.Nyerere hakwenda kwenye uhuru wa Zimbabwe. Alikwenda baadaye ziarani. Nasikia alimwambia Mugabe: 'You have inherited a jewel, keep it that way.'
jokaKuu,
Ukishakuwa mtu mashuhuri lazima kuwepo na stori za vijiweni. Ni kama ile stori ya Nyerere kumpa Malkia Elizabeth kifimbo chake badala ya kushika mkono wake. Nina hakika umeshasikia stori nyingi juu ya Kawawa.
Kama aliyasema hayo basi ni maneno ya kisiasa kutoka kwa mwanasiasa! hivyo hayana uzito wowote kwangu mimi.
Ningependa kujua sababu zilizomfanya kwa nini asiende Zimbabwe siku ya Uhuru?
BAK,
..Thank u.
..I try to be accurate lakini mara nyingine huwa nachemsha.
..In this particular case, kidogo niingie mkenge wa kuanza kubishana na Kiranga.
..namshukuru Jasusi kwa kuni-bail out. LOL!!
NB:
..ila kuna watu wameshatoana ngeu hapa JF kwa kubishana kwamba Mwalimu alikataa kumpa mkono Bob Marley siku ya uhuru wa Zimbabwe.
..sasa imejulikana kwamba habari hiyo ni URONGO kwasababu Mwalimu siku hiyo tajwa alikuwa Dar-Es-Salaam.
..mimi nasema u can lie anywhere else but not at JF.
Najua hii utaipiga chenga. Je kwanini JKN alitengana na mama Maria?