Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Nyie haya mambo yakubeti mtu asije kusubutu kama anajua hela yake ni ya mawazo
Jana ilikua nusu nife kwa presha kwasababu ya betting. Sikuhiyo nimekaa na mtu wangu waheshima kabisa ninayemuheshimu, katika story za hapa napale nikamwambia aisee madirisha yangu yapo kwa fundi alafu sina hela hapa ninamilion nne tu. Akaanza kuniambia mbetie Simba afungwe bao tatu na mwarabu kule Morocco ukiweka milion nne unapata milion 16 unamaliza mambo yako.
Basi bwana nikajikuta nimeanza kushawishika kwakile anachoniambia ndg yangu. Nikaanza kuona Simba nimbovu kweli lazima afungwe tano maana wale wydad Casablanca siyo poa wakiwa Morocco. Nikamwambia nielekeza jinsi ya kubeti niweke hela hii game Simba anakufa nyingi. Basi akanielekeza nikaweka million tatu Simba afungwe goal zaidi ya nne ambayo hapo ningepata milion 12.
Oya mpira umeanza nimekaa na washkaji sehemu moyoni naombea Simba apasuke chuma nyingi nipate hela. Mpira umeenda mpaka dakika 45 hakuna bao Simba kakaza. Nikaanza kuhisi kijasho chembamba kinanitoka. Naanza kuiwazia milion tatu yangu inapotea ndani ya dakika 45. Nikaona kama pumzi inakata nikaagiza pepsi kwanza nishushe presha. Dakika 45 za kipindi cha pili zikaanza Simba anazuia yani natamani niingie uwanjani niwafunge miguu wafungwe hata bao kumi ila ndiyo sina uwezo huo.
Dakika ya 70 ngoma bila bila. Nikaanza kujisikia vibaya yani nahema kwa tabu sana jasho jingi nahisi joto sana na wakati hakukuwa na joto. Dakika ya 80 bado hakuna bao na hapo ujue mkeka unataka bao tano ndiyo nipate hiyo hela. Dakika ya 85 nikazimia. Nimekuja kushtuka nipo hospital na drip mkononi. Ile nimezinduka namkuta broo kakaa pembeni yangu anasikitika kinafiki wakati yeye ndiye kanishauri. Namuuliza vipi broo ngap ngap? Anatikisa kichwa anasema mkeka umechanika. Alivyosema hivyo nikazimia tena.
Oya nilikaa pale hospital siku tatu presha inapanda wakiishusha inashuka jumla wakiipandisha inapanda jumla.
Yani kila nikiwaza million tatu yangu presha inapanda. Basi broo akaona nitakufa akaenda kutafuta hela huko kaniletea kaniambia mdogo wangu punguza mawazo hela yako hii hapa haijapotea. Hapo kidogo nikaanza kujisikia nafuu kesho yake nikaruhusiwa kurudi nyumbani. Tangu hapo nikiona mtu anabeti nahisi kama anataka kujiua.