Mtu Asiyejulikana
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 2,254
- 5,161
"MASHABIKI WA SIMBA MSIKUBALI KUINGIZWA KWENYE MAPRESHA YASIYO NA SABABU.
Mafanikio ya mpira huwa ni process vinginevyo labda iwe fluku.
Kwenye mpira fluku ipo. Ligi ya Uingereza Leicester ilikutana na fluku ikatwaa ubingwa na baada ya hapo misimu miwili mbele ilishuka daraja.
Unaweza kupata Fluku msimu mmoja ukafika fainali ya shirikisho ila Kwa kuwa ni fluku misimu miwili mbele ukashindwa kuvuka makundi.
Kuna presha inatengenezewa mashabiki wa Simba kwamba Sasa ionekane kucheza robo fainali ni hatua ndogo na haina faida yoyote bali mnatakiwa kufika fainali sababu tu kuna waliofika Kwa fluku.
Mkiikubali hiyo presha na mkasahau zaidi 70% ya wachezaji wenu ndio kwanza msimu wakwanza wanacheza Simba na mkasahau hata benchi la ufundi ni jipya na ndio kwanza linaitafuta Simba tunayoitaka. Ni kwamba ghafla mtahama kuwa wavumilivu na timu yenu na mkaanza kudai mafanikio ambayo yatakuwa ni sawa na kutaka kuhamia nyumba mpya ambayo haijakamilika kujengwa.
Ukiniuliza Mimi nitakwambia timu ipo kwenye njia sahii ya kujengwa upya na hapa tulipo tunakula bonus ambayo Wala hatukuitarajia.
Tunachopaswa kufanya Kwa Sasa ni kuiunga mkono timu yetu Kwa nguvu zote na kuipambania iendelee kufanya vizuri bila kuwapa presha yoyote viongozi, benchi la ufundi Wala wachezaji.
Tukikubali kujazwa upepo wa presha na tukaanza kupeleka presha Kwa benchi la ufundi na wachezaji tukawaondolea utulivu wakaanza kucheza Kwa presha ya matokeo na kulazimisha mambo tutaharibu.
Kwa Sasa lazima tukubali Simba imetuheshimisha na tuendelee kuwapa morali wachezaji wetu waendelee kupambana wakijua tupo nyuma Yao katika mazingira yoyote bila kuwapa presha hata chembe.
Tuwaache wanaopenda fluku waendelee kusubiri fluku nyingine huku sisi tukikubali mpira ni process na tunajua taratibu tutafika tunapokwenda. Tulitengeneza timu iliyotupa mafanikio ikafika mahali ikafika mwisho ikachoka na tukaibomoa. Imetuchukua misimu mitatu kuanza kuona timu mpya yenye matumaini inajengwa upya.
Tuweni na subira na tusikubali kabisa kutiwa ndimu na wanaotaka kututia presha tuanze kuhamaki na kuhama kwenye lengo.
SIMBA BADO INAJENGWA NA MASHABIKI WA SIMBA TUNAJUA HILO NA TUTAENDELEA KUWA NA SUBIRA
(Jicho la tatu la Mgalilaya).*