Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Hebu angalia hiyo picha hapo chini. Ona hao watoto walivyorundikana humo darasani. Ona walivyobanana kwenye hayo madawati. Angalia hao walio sakafuni.
Wengine wameinama sijui hata kwa nini. Labda migongo inawauma.
Jamani hivi sisi ni majuha kiasi cha kushindwa hata kutengeneza mazingira yenye ahueni ambayo wanetu watasoma bila kuteseka? Sitaki kuamini tu majuha kiasi hicho lakini sina jinsi. Watu gani wenye akili wataruhusu watoto wao wasomee kwenye mazingira kama hayo? Nyambaaaf kabisa.
Hivi kujenga madarasa mazuri yenye kupendeza na yenye viti au madawati ya kutosha ni sawa kweli na kutengeneza maroketi ya kwenda angani na huko kwenye sayari zingine? Ni wazi jibu hapo si sawa. Sasa unahitaji uwe na akili kiasi gani ili uweze kuboresha mazingira ya kusomea wanao? Hakika huhitaji akili kama za kutengeneza maroketi.
Sayansi ya maroketi ni fani iliyo changamani (complicated) zaidi na yenye kuhitaji umakini wa hali ya juu. Ugumu wa kujenga shule nzuri zenye vifaa vya kutosha uko wapi? Nielezeni mwenzenu maana nimefikiria weee hadi nimeanza kuona kizunguzungu. Sioni ugumu uko wapi lakini naona ni wazi kuwa hatuwezi. Nazidi kuchanganyikiwa kabisa.
Sisi ni watu wa ajabu sana. Viongozi wetu wanaishi maisha ya hali ya juu sana. Wanajifanya wanajali watu wawaongozao. Waongo wakubwa hao. Hawajali chochote. Wangekuwa wanajali walahi tena hali kama za hili darasa hapo chini zisingekuwepo.
Kazi kusafiri na kununua magari ya bei mbaya kila kukicha. Hawaishi kutumia mihela kibao (mibilioni) kufanyia 'ukarabati' makazi yao yenye mabwawa ya kuogelea huku kuna watoto wa shule wanakalia sakafuni wakivuta na kupumua hewa yenye mavumbi. Ni utu kweli huu?
Badilikeni nyie watawala. Kuweni na mioyo ya kibinadamu. Sio vizuri kuishi maisha ya anasa kwa kutumia hela za walipa kodi walio masikini huku mkiwaacha hao walipa kodi waishi kama si binadamu. Wajalini watu mnaowaongoza.