Nyimbo za hivi karibuni za vijana wa Yamoto band ni moto wa kuotea mbali... Nani kawafunika wenzake?

Nyimbo za hivi karibuni za vijana wa Yamoto band ni moto wa kuotea mbali... Nani kawafunika wenzake?

Dong Jin

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2018
Posts
968
Reaction score
2,034
Yamoto band ni kundi lililotikisa sana miaka michache ya nyuma hapa bongo... liliundwa na vijana machachari wenye mashairi pendwa kwa rika zote. Baada ya hilo kundi kuvunjika kila msanii alianza kutoa nyimbo zake kama solo artiste... alianza aslay, huyu hakuna haja ya kumuongelea saana maana shughuri yake kila mtu anaijua. Akaja beka flavour tukamsikia jinsi alivoufanyia haki wimbo wake "libebe"... Akfuatia enock bella de benz, tuliona jinsi alivoingia vizuri na ngoma yake ya kwanza ya "Amida"... Maromboso aka mbossokhan akaja baadae naye akatoa "watakubali" iliyomtambulisha vyema mtaani... Tuachane na hayo twende kwenye maada kuu...

Kipindi hiki cha mwezi huu wa tisa tumeona vijana wa yamoto wameona huu mwezi usiende bure bila kuweka kazi zao masikioni mwa watu...
Alianza beka flavour kuachia wimbo wake wa SIWEZI,
Akaja enock na GOIGOI,
Aslay naye hakubaki nyuma akatuletea KWATU,
Kama hiyo haitosh na mbosso naye akajibu mashambulizi kwa HODARI....
Nimeshindwa kuziambatanisha hizo nyimbo zao lakini kila mtu najua atakuwa kazisikia.
Je ni nani kawafunika wenzake kuanzia sauti, mashairi, beat, nk? Shusha maoni yako hapa...
 
kijana nlikua namkubali alivokua ya moto alivoenda wasafi nlikua naona anaimba utumbo lakini Siku hizi daah yy ni hodari kuliko wote
mbosso-hodari-1-640x640.jpg
 
Back
Top Bottom