Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 8,632
- 23,673
Binafsi sio mpenzi sana wa miziki ya kisasa ila nimezisoma sana miziki ya miaka ya 1930s mpaka 1980s na hata ya 1990s na navutiwa sana na aina hii ya miziki ikiwa kwenye ujumbe na burudani pia. Miziki ya 2000s nimesikiliza sana kabla ya 2012 ila mingi baada ya hapo naisikia sikia tu nimekuwa kidogo nje ya mziki wa kisasa.
Leo nikiwa natoka morogoro nikiwa kwenye coaster basi dereva akawa anapiga nyimbo za msanii anaitwa Mboso. Kwa kweli nimekuwa makini nikisikiliza mziki wa huyu msanii njia nzima mpaka naingia mbezi. Kufika Kijiji chas Mwidu kilichopo Ubena Zomoni nikajikuta njaa inauma sana kwa sababu ya mziki wa huyu jamaa.
Niko kwenye mfungo wa kwaresma na sijafungulia hata moja isipokuwa ya leo. Nilipoingia Chalinze tu nikajisikia utumbo unakwaruza nikajikuta nimenunua chips ili nipunguze njaa. Safari ikaendelea dereva anamkubali sana huyu jamaa au flash ilikuwa na nyimbo za Mboso tu, ile kufika Ruvu tumbo lilikuwa linanguruma mpaka abiria aliyekaa pembeni yangu akawa ananitolea macho sana. Ikabidi ninunue mahindi ya kuchoma nile kupunguza njaa.
Hizi nyimbo za huyu msanii zimenifanya nikasikia njaa sana, akiimba kidogo mara, wa mafuuta ya karafuu Nikichoka ananikanda kwa mabarafu Maajabu maajabu, penzi lake la ajabu Maajabu, yani nilipofika Mlandizi hujui kuwa una genye au una njaa.