Nyimbo za vigodoro kwenye jukwaa la kimataifa la AFL ni ushamba

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Nilishangaa sana kuimbwa kwa nyimbo yenye maudhui ya mke mtu sumu kwenye ufunguzi wa jukwaa kubwa kama la African Football League linalotazamwa na dunia nzima.

Kuweka nyimbo za vigodoro kwenye jukwaa kubwa hivi tulifeli pakubwa sana na kujiaibisha. Nyimbo za kuweka katika majukwaa ya kimataifa zinapaswa kuwa classic na kuonyesha hali ya uki-mataifa.
 
Nilishangaa sana kuimbwa kwa nyimbo yenye maudhui ya mke mtu sumu kwenye ufunguzi wa jukwaa kubwa kama la African Football League linalotazamwa na dunia nzima...
Huwezi kufanikiwa kwa kuiga Iga, miziki ya uswazi kama Singeli ni katika miziki ambayo ni OG kabisa. Mtu yoyote kimataifa akiusikiliza lazima ahisi hiki kitu kipya.
 
CAF walisema wanataka msanii mmoja tu Simba wakapendekeza Ali kiba.CAF wakamwambia Alikiba apeleke nyimbo Tano basi nyimbo waliyochagua ni hiyo sumu kati ya hizo Tano.Ile shughuli imeratibiwa na CAF.Alikiba alipewa masharti nyimbo yake aimbe Kwa Dk 2 ma sec17 awe ameshamaliza.ndo maana uliona mambo yanaenda fasta fasta alivomaliza kapewa kibunda chake akapita hivi.
 
hata yule mbana pua kiba hana hadhi ya kutumbuiza kwenye shughuli kama ile. mjombamjomba angefaa zaidi.
 
Huwezi kufanikiwa kwa kuiga Iga, miziki ya uswazi kama Singeli ni katika miziki ambayo ni OG kabisa. Mtu yoyote kimataifa akiusikiliza lazima ahisi hiki kitu kipya.
Sijasema tuige mahali, pia mzuki kuwa OG haina maana ni mzuri au unakidhi kiwango cha kimataifa, unaweza kuwa ni utumbo tu pia . Nchi zilizoendelea anakotoka Infantino mke wa mtu sio sumu.
 
Wabongo hawajisumbuagi kuumiza kichwa ili kuleta kilicho Bora machoni pa watu na kimataifa, hawanaga jicho la Mbali kbs kwenye mambo muhimu km hayo

Yani sio viongoz wa serikali yetu, sio wasanii yan wte ni mambumbumbu all time
 
Lakini mwenzio kashapata maokoto na leo lazima familia yake imekula vizuri plus chawa wake .

The rest is history
Sizungumzi suala la maokoto, hata mafisadi malaya, na majambazi wanapata maokoto.
 
Nazungumzia maudhui,
Mke wa mtu sumu haina universality, ni mambo ya Kiswahili zaidi.
Muziki siyo ujumbe tu! Muziki ni mdundo, sauti, ujumbe, nk. Kama ingekuwa muziki ni ujumbe pekee, basi vijana wa zamani kama sisi tusingeipenda miziki ya Wakongomani, ya Kihindi, ya Kizungu, nk!

Imagine Wakongomani wanaimba kwa lugha ya Kilingala na Kifaransa, lakini mwisho wa siku tuliipenda!! Imahine katika wimbo unasikia tu maneno kama bolingo nangai, sheli nangai, nk. Lakini mdundo na sauti, vilitufurahisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…