Nyoka Anammeza Kangaroo

Nyoka anaonekana mdogo ......duu hili dubwana ukikutana nalo kwenye misitu ya nyika ni balaaa! Sijui kama wanaweza kimbiza prey maana nitakimbia kuliko Magic Johnson
 
Hii ni njaa au umaarufu??

Heshima kwako Ngoshwe.

Umeuliza swali zuri ingawa nimeona wanajamvi wamekupa wajibu mepesi pengine kwa kukufurahisha au kutokujua.Huyu ni nyoka aina ya chatu na kwa kweli huo ni mloo wake wa kawaida kabisa.Kwanza anaanza kwa kukamata windo lake halafu anakubana kwa kujisokota kwenye mwili wa mnyama ili kukuvunja vunja na baadae anakumeza taratibu.Baada ya hapo atakaa muda mrefu sana bila kula chakula chochote sikumbuki vizuri lakini anaweza kukaa hata miezi mitatu.

Ukifanya mahesabu ya haraka haraka kuanzia muda anaochukua baada ya kula chakula mpaka siku atakapotafuta chakula kingine kwa kweli hakuna kitu cha hajabu.
 


Duh mbona una experience hivo, uliwahi kuliwa nini
 
Kwa muono wangu ni kuwa inawezekana huo ukawa ni mlo wake wa kawaida lakini uroho wake huo unamfanya awe vulnerable kwa hata adui mdogo ambaye kwa kawaida asingefikiria kupambana naye kwa hali aliyonayo anakuwa hana uwezo wa kujihami.
Ujumbe: UROHO UNAWEZA KUKUTOA ROHO
 
Duh mbona una experience hivo, uliwahi kuliwa nini

Heshima kwako BabaBabuu,

Umenifanya nikacheka sana leo.Mkuu wangu mara nyingi napenda kuangalia vipindi vya wanyama nimejifunza mambo mengi sana kuhusu wanyama wa aina mbali mbali Chatu akiwa ni mmojawapo ingawa niliangalkia kipindi kirefu kilichopita labda mwaka 2001.
 

hapo kwenye nyekundu naomba nikusahihishe kidogo, anapojisokota sio kama anakuvunjavunja, ila anachofanya ni kusense jinsi unavyopumua, kwa hiyo kila unapota hewa nje yeye anabada kidogo, inafikia point anakuwa amekubana kabisa kiasi kwamba kunakuwa hakuna space ya hewa kwenye mapafu yako na unakufa kwa kukosa hewa, nadhani hata ukiangalia hiyo picha utaona huyo kangaroo bado anaonekana na kitambi chake kama kawaida, kwa hiyo amekufa kwa kukosa hewa baada ya kubanwa sana. maelezo mengine nadhani ni sahihi
 

Heshima kwako Kituko.

Nimekupata mkuu maelezo yako yako sahihi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…