SI KWELI Nyoka wa kijani ni Wambea, husikiliza maongezi ya watu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.


HII NI UZUSHI NA HADITHI TU YA JADI.

Nyoka wa kijani hawana tabia ya kusikiliza mazungumzo ya watu kwa kujificha.
Mara nyingi wanapatikana juu ya miti kwa sababu wanapenda mazingira hayo kwa ajili ya kujificha na kuwinda chakula.
Kama nyoka ataanguka kutoka mti, inaweza kuwa kwa sababu ya kushtuka, kugusa kwa bahati mbaya, au sababu nyingine za kimaumbile, lakini si kwa sababu ya kusikiliza umbea au mazungumzo ya watu.

Hadithi hizi zinaweza kuwa zimeundwa kwa nia ya kutoa mafunzo fulani au kama sehemu ya utamaduni wa hadithi za kuburudisha.
 
Asante JamiiCheck nimejifunza kitu kupitia huu uzi.

PIa, umeniongezea siku za kuishi maana nimecheka hatari kusikia nyoka anakuwa mbeya🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…