Nyoka wenye mistari wana madhara?

Nyoka wenye mistari wana madhara?

Dafugwadu

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
4,688
Reaction score
5,129
Wajumbe habari za muda huu?

Niko njiani natembea kurudi zangu nyumbani kutoka kilimoni. Hatua mbili mbele kakatisha mjusi wa mistari mistari. Nilivyopiga hatua sijakaa sawa kapita nyoka huyo wa mistari katikati ya miguu yangu akaunga kule alipokimbilia mjusi.

Uongo mbaya niliishiwa nguvu na miguu ikawa inatetemeka mno. Nilivyokaa sawa mtaji mbio ila hajaniuma popote.
 
Madhara wanayo kama nyoka wengine tu, ila nasikiaga hawana tabia ya ukorofi wanapenda kujiami kwa mbio. Na nadhani wapo kwenye orodha ya nyoka wenye speed kubwa
 
Hao nyoka wa mistari wana tabia hizo za kukatiza miguuni unapotembea. Sijawahi kusikia wameng'ata
Mtu. Mwanza wapo wengi
 
Hao nyoka wa mistari wana tabia hizo za kukatiza miguuni unapotembea. Sijawahi kusikia wameng'ata
Mtu. Mwanza wapo wengi
Ameniletea mbwembwe hapo miguuni ikabidi nitulie, na sio ujasiri hapana miguu iligoma kufanya chochote.
 
Unavyohisi huyo mjusi na nyoka ni washkaji tu au kunalaziada linaendelea maana wanatokaje kichakani wanafuatana,kunakitu walikuwa wanafanya wewe ndio umewakurupua
 
Unavyohisi huyo mjusi na nyoka ni washkaji tu au kunalaziada linaendelea maana wanatokaje kichakani wanafuatana,kunakitu walikuwa wanafanya wewe ndio umewakurupua
Nimerudi nyumbani chap ikanibidi niingie chimbo.
Hapa nimeangalia nikaona huyu snake wa mistari yule mjusi ndio chakula chake, amemsokota akammeza full
 
Back
Top Bottom