NYONGEZA: Huyu ndiye Earle Edward Seaton

NYONGEZA: Huyu ndiye Earle Edward Seaton

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NYONGEZA: Huyu ndiye Earle Edward Seaton kama anavyoelezwa na Abdul Sykes:

"Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyika chini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Kama mamlaka tawala Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala.

Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo.

Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwa wengi na wenye nchi.

Labda kwa kuanua ngoma juani, Gavana Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya ustawi wa jamii na Native Authorities, kutaka mapendekezo ya jinsi Tanganyika itakavyotawaliwa.

Kamati ya siasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ya siasa: Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Sheikh Said Chaurembo.

Katika taarifa yake ya mwaka ya 1950 Abdul Sykes aliandika maneno haya:

"Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria.

Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi.

Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba"
 
Back
Top Bottom