MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Naona nchi haiwezi kuhema bila Erasto Nyoni na Kelvin Yondani kwenye ulinzi. Hawa wachezaji waliomba kustaafu kuchezea timu ya taifa lakini ikabidi waombwe kuendelea sababu ya kukosa mbadala.
Ushauri wa bure ni kuomba Simba wamtumie Mlipili badala ya Nyoni kucheza hata me mechi ambazo hazina pressure. Tunahitaji mbadala wa Nyoni na Yondani haraka kabla miili yao haijagoma kucheza.
Hakuna eneo Tanzania ina hatari kubwa kama eneo la ulinzi kuwakosa Nyoni na Yondani kwa pamoja. Watu wa mpira angalieni namna ya kuziba haya mapengo kabla hayajawa mapengo.
Tutoe nafasi kwa akina Ally Mtoni, Mwantika na Mlipili ili wajiandae kuziba nafasi za hawa wakongwe kabla miili yao haijagoma tuanze kuwalaumu wakati waliomba wapumzike.
Erasto Nyoni na Kelvin Yondani ni pair ambayo kuitengeneza nyingine ni safari ndefu sana. Tujipange mapema