Nyoni na Yondani tegemeo wasio na mbadala

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Naona nchi haiwezi kuhema bila Erasto Nyoni na Kelvin Yondani kwenye ulinzi. Hawa wachezaji waliomba kustaafu kuchezea timu ya taifa lakini ikabidi waombwe kuendelea sababu ya kukosa mbadala.

Ushauri wa bure ni kuomba Simba wamtumie Mlipili badala ya Nyoni kucheza hata me mechi ambazo hazina pressure. Tunahitaji mbadala wa Nyoni na Yondani haraka kabla miili yao haijagoma kucheza.

Hakuna eneo Tanzania ina hatari kubwa kama eneo la ulinzi kuwakosa Nyoni na Yondani kwa pamoja. Watu wa mpira angalieni namna ya kuziba haya mapengo kabla hayajawa mapengo.

Tutoe nafasi kwa akina Ally Mtoni, Mwantika na Mlipili ili wajiandae kuziba nafasi za hawa wakongwe kabla miili yao haijagoma tuanze kuwalaumu wakati waliomba wapumzike.

Erasto Nyoni na Kelvin Yondani ni pair ambayo kuitengeneza nyingine ni safari ndefu sana. Tujipange mapema
 
Umesema kweli... ila watapatikana tu japo itawachukua muda kucover vzr
 
Ila mkude kama amechuja sio mkude wa kipindi kile afu wabongo haya mambo ya kukariri nyumbani ndo mahala pakufanya vizuri yanatugharimu sana mfano leo stars toka mwanzo wanacheza kama vile wanaongoza kwa goals kadhaa .
 

Ni ajabu leo nimeangalia mpira huo na nimeona kuwa Yondani na Nyoni hawawezi tena na hawana pumzi ya kwenda sambamba na mziki wa vijana wa leo au niseme "wamezeeka" wanatakiwa wapumzike huko kwenye timu zao
 
Bora ya huyo Mlipili ila siyo Sonso na Mwantika. Ni wazito sana kiakili na pia kimwili. Sema kuna mabeki wengi sana na bora ndani ya ligi yetu! Tatizo ni kule kucheza kwao kwenye timu ndogo kama Ruvu Shooting, Polisi Tanzania, nk.
 
Write your reply...Ngoja ninja apate uzoefu atakuja kutusaidia.
Sawa, huyu akipata uzoefu na kuacha ule uninja usiokuwa na maana anaweza kuwa mzuri. Lakini ingefaa zaidi tukipata beki mwingine mwenye asili ya bara kwa manufaa ya kilimanjalo stars.
 
Mpira wa tanzania nafatilia sana sema kukalili majina inanipa shida kidogo ila kwenye ulinzi Abdalah Shaibu ninja, Paul Godfrey Boxer na Mohamed Hussein zimbwe Junior pamoja na Hassan Kessy Ramadhan bado ni Vijana wenye Future kubwa mbeleni
 
Kuna beki mmoja mpemba alikua anachezea KMC anaitwa Aly Aly.. yule akipewa hata elfu 50 atahakikisha anajifunga tena hadi ma free header anatupia tu golini kwake.. kweli mabeki wanaojitambua wameisha
 
Right.
Nikiona arsenal tunahangaika na beki hakika nakuelewa vyema.
 
Ni ajabu leo nimeangalia mpira huo na nimeona kuwa Yondani na Nyoni hawawezi tena na hawana pumzi ya kwenda sambamba na mziki wa vijana wa leo au niseme "wamezeeka" wanatakiwa wapumzike huko kwenye timu zao
Ila ndio tegemeo, ikitokea ghafla wote wasicheze ni aibu pale kwenye ulinzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…