Kikosi cha Simba kitasafiri Alfajiri ya December 5, 2024 kwenda Algeria ambapo itacheza mchezo wa pili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine.
View attachment 3168396
Kikosi kitaondoka na nyota 22 kuzisaka pointi tatu nyingine kwenye Uwanja wa Mohamed Halaoui Desemba 8 kuanzia saa 1:00 Usiku.
View attachment 3168394
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa timu zote mbili ikiwa simba ilicheza mchezo wa kwanza dhidi ya FC Bravos na kushinda kwa bao 1-0 huku CS Constantine ikishinda dhidi ya CS Sfaxien kwa bao 1-0
Msimamo wa kundi A upo hivi:
1. CS Constantine - 3
2. Simba SC - 3
3. FC Bravos - 0
4. CS Sfaxien - 0
Namba ni alama walizovuna kwenye mechi ya kwanza.