Nyota 5 'wa Kimataifa' wa Simba SC kulitetemesha bara La Afrika.

Man of the match.. Ni Okwi.. Goal 2.. Assist 1.
 
Ile kazi ya Nyota wa Kimataifa wa Simba SC tuliyowatuma wanaimaliza leo (16/10/2018), ambapo..

1. Haruna Niyonzima na MK14 watakua dimbani wakilipambania taifa lao dhidi ya Guinea.. Ikumbukwe mechi iliyopita Rwanda walifungwa 2-0 kwa msaada mkubwa wa Refa.. Sasa leo Guinea lazima wakione cha moto.
2. CR7 wa Uganda pamoja na Juuko Murshidi watakua dimbani wakimalizia kazi waliyoianza wiki iliyopita pale watakapokua ugenini wakipambana na Lesotho.. Ikumbukwe mechi iliyopita Lesotho alikung'untwa goli 3-0 huku CR7 wa Uganda, Okwi akiingia kambani mara 2.. Sasa leo kuna hatari mtu akapigwa mkono.. Huku o
Okwi akiondoka na mpira wake.

Baki hapa hapa 4 more updates.
 
Hatimae mechi za Kimataifa zimekamilika, na yafuatayo ni maelezo juu ya performance za wachezaji wa Simba SC waliokua wakitumikia mataifa yao;

1. Emanuel Anord Okwi
Huyu jamaa kacheza mechi zote 2.. Kafunga goli 2, assist 2, kasababisha penalty pia alikua man of the match katika mechi 1.

2. Juuko Murshid
Beki huyu kisiki kacheza mechi 2.. Na kaisaidia timu yake ya Taifa ya Uganda kushinda mechi zote, huku akihakikisha timu haifungwi goli lolote.

3. Clatous Chota Chama
Kiungo bora kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini Zambia, alicheza nae mechi zote 2. Aliasist goli 1 huku akiibuka man of the match katika mechi 1.

4. Haruna Niyonzima
Kiungo huyu machachari toka nchini Rwanda, aliitumikia nchi yake katika mechi 2.. Huku akiasist goli 1.

5. Meddie Kagere
Goal Machine, MK14 pamoja na mabeki kumkamia sana.. Aliasist goli 1 katika mechi 2 alizocheza.

CONCLUSION:
Kwa viwango walivyoonesha hawa wachezaji katika kipindi hiki, ama kweli bara la Africa lilitikisika.
Tukutane next time. Ahsanteni.
 
Wale wachezaji wamesaidia timu zao kushika nafasi hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…