Nyota angani zimepotelea wapi? Wanajiografia tusaidie

Nyota angani zimepotelea wapi? Wanajiografia tusaidie

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Habari ndugu wanaJF,

Zamani tunakua ilikuwa anga likiwa bright hasa nyakati za usiku, wakati unasubiri chakula cha usiku ili usisinzie baba alikuwa anatuambia nenda kahesabu nyota na zilikuwa nyingi mno na zilikuwa zikionekana katika makundi.
Sasa je, siku hizi zimekwenda wapi? Au Ni Mimi ndio mhenga?
 
Hapa nilipo naziona km nne angani,labda kila mtu anakufa na nyota yakee!!!
 
Kuna nyota zinazunguka dunia kwa muda mrefu ndio zitokeze tena kama mwezi unavyopotea na kutoka tena. Nyota zingine huchukua miaka mingi kuzunguka dunia.
 
Kuna nyota zinazunguka dunia kwa muda mrefu ndio zitokeze tena kama mwezi unavyopotea na kutoka tena. Nyota zingine huchukua miaka mingi kuzunguka dunia
umeandika kama vile unajua kumbe ni konyagi na ugoro. NYOTA ZINAIZUNGUKA DUNIA?
 
Umeuliza swali zuri sana. Kwanza sijui upo mjini au maeneo ya vijijini? Ipo hivi.

Nyota huonekana vizuri sana km ukiwa maeneo yenye kiza kinene yasiyo na taa nyingi. Sasa siku hizi miji imekuwa kwa kasi sana,umeme umeenea sehemu nyingi.Mwanga wa bulb majumbani, taa za barabarani na taa za magari vyote kwa pamoja vinapunguza uangavu wa nyota kwa kiasi kikubwa. Ndio maana wanasayansi wanashauri km mtu anataka kutazama au kujifunza kuhusu nyota aende nje ya mji hasa porini.
 
Kwa sisi wahenga "Chakula cha usiku" ni relative term.

Ngoja niangalie angani nithibitishe.... Japo sijajua hiyo "zamani" unayoizungumzia ni zamani ya miaka ipi....
Hadi miaka ya 1990 hata mi nilikua naziona hadi vimondo
 
Kuna nyota zinazunguka dunia kwa muda mrefu ndio zitokeze tena kama mwezi unavyopotea na kutoka tena. Nyota zingine huchukua miaka mingi kuzunguka dunia
Kwahiyo Mkuu ndugu yangu unataka kuniambia kwakuwa kuna kuoatwa kwa mwezi basi pia kuna kupatwa kwa nyota?

Binafsi leo ndio mara yankwanza kusikia kumbe nyota nazo zinazuiguka dunia.

Kumbe hii dunia inazungukwa na vingi sana ndo maana shujaa Majaliwa aliweza kuufungua mlango wa ndege kwa makasia mpaka akafanikiwa kuwapungia mkono marubani.
 
Ukitaka kuona nyota kwa wingi na ung'avu wake nenda eneo ama mji ambao Marope anapractize katafunua ya nguvu. Mazingira ya giza yanakuwezesha kuona anga vyema na unaweza kuzihesabu nyota ukitaka
 
Back
Top Bottom