Nyota ni nini?

Nyota ni nini?

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
MADA: ASTROLOGY

MKUFUNZI: Dr. Rwakiunge Rugambwa (PhD)

UTANGULIZI:

Nyota ni nini?

Mara nyingi tunasikia watu huko nje au kila mahali wanazungumzia Nyota, Nyota, Nyota; lakini wanakuwa wakimaanisha nini hasa?

Je, nyota ni nini?

Kuna mitazamo tofauti kuhusu elimu ya Nyota.
Wapo wanaoiunga mkono elimu hii na wanajua ndio msingi wa maisha ya binadamu na viumbe vingine vyote, lakini wapo pia wanaoichukulia kama uchawi na elimu isiyofaa kabisa!

Wote wapo sahihi maana Kanuni za maumbile zinatufundisha kuwa kila palipo na positive, kuna na negative pia.
Palipo na nuru kuna na giza pia.
Palipo na Hasi lazima kuwe na CHANYA pia ili maisha yawe neutralized.
Kwa hiyo kwa mujibu wa sheria za maumbile, kila mtazamo wa mtu kwenye kitu chochote, ni sahihi kwake mwenyewe na kwenye maumbile (tunaita the law of Duality)

Elimu ya Nyota ni elimu kongwe zaidi kuliko elimu zote zilizopo leo.
Ni kongwe kuliko hata Elimu ya viumbe (Biology), kuliko Elimu ya mambo ya dini (Theology) na elimu nyinginezo mnazozifahamu, zile zilizopo leo, kama Archeology, Physiology, Psychology, Ecology nk.

Hii elimu ya Nyota ni kati ya elimu za kale na kale zilizotumiwa na wanadamu wa kale kuendesha maisha yao.
Ya kwanza ikiwa Symbology (Elimu ya alama/ ishara) Numerology (Elimu ya namba) ikifuatiwa na Sacred Geometry (Elimu ya michoro) na kisha Astrology!

Astrology ni nini?

Astrology ni neno la kiyunani (Greek word) linalomaanisha Elimu ya viumbe vya angani.

Ni muunganiko wa maneno Astrón + Logos.

Astrón (au astral) ni kuelea angani na hasa anga za mbali (nje ya sayari ya dunia)
Logos ni "Elimu ya" (yaani the Study of)

Kwa hiyo tunapozungumzia Elimu ya Nyota, tunazungumzia Elimu ya viumbe (vya kiroho), vinavyoelea kwenye anga za mbali.

Kwa kusema hivyo, tunamaanisha Nyota ni viumbe vya kiroho, vinaishi kwenye anga za mbali, ambako kwenye dini tumezoea kuita mbinguni!

Kama ilivyo sheria ya "as above so below" (kwa tafsiri isiyo rasmi "duniani kama mbinguni") basi viumbe vyote vilivyopo duniani vimeunganishwa na hivyo viumbe vya angani (the Law of Divine Oneness)

Ni sawa na kusema kila kiumbe cha angani (au mbinguni, kwa lugha ya kidini) kinahusiana moja kwa moja na kiumbe kilichopo duniani.

Ulimwengu wa anga za mbali (Higher Dimensions or Heavenly realms) ni mkongwe zaidi kuliko ulimwengu huu tunaoishi sisi wanadamu, ulikuwepo kabla ya huu tuliomo sisi.
Maana yake hata viumbe (beings) vilivyokuwa huko ni vikongwe zaidi kuliko vilivyopo huku.

Kwenye mada ya ABIOGENESIS (chanzo cha Uhai) tunajifunza kwamba maisha ni mzunguko, yaani roho huvaa mwili kisha huuvua na kurudia asili yake na baadaye huuvaa tena, yaani urejea kwenye mwili na kisha kuuvua na huendelea hivyo hivyo to the infinity. Hii tunajifunza kwenye kipengele cha reincarnation, kwenye mada ya Abiogenesis.

Nataka kusema kwamba viumbe vilivyopo kwenye anga za mbali au viumbe vya kiroho, ambavyo ndio hasa NYOTA ZENYEWE, uwa vina-shift dimensions na kuja duniani (kuvaa miili/ kuzaliwa) na kisha kurejea kwenye asili yake (kufa) na hii ndiyo maana ya mtu kuitwa nyota!

Mtu kimsingi ni Nyota.
Yaani ni Nyota iliyovaa mwili.
Uwa napenda kusema, mtu ni nyota na nyota ni mtu.
Mtu na nyota sio tu umoja, bali ni kitu kimoja!

Alikuwepo kabla hajakuwepo na ataendelea kuwepo hata baada ya kutokuwepo.

Yaani wewe hapo kabla hujazaliwa ulikuwepo na hata utakapoondoka kwenye mwili huo (kufa) utaendelea kuwepo.

Acha nitoe mifano kutoka kwenye maandiko ya Kitabu kinachoitwa Biblia, lakini nieleze sababu kwa nini uwa masomo yangu yote yana msingi kwenye Biblia.

Biblia (The Bible kwa Kiingereza) ni neno la Kiyunani, lilitoholewa kutokana na neno 'Biblós' which means THE COLLECTION OF BOOKS (mkusanyiko wa vitabu)

Huu ni mkusanyiko wa vitabu vya kale zaidi, vitabu vikongwe zaidi kutoka Kemet, Sumeria, Canaan, Persia na Israel.

Warumi walivi- edit na kuviweka pamoja kwa maslahi ya Dola yao (Roman Empire)

Ni wazo lililotokana na Mwanafalsafa wa kale Aristotle, alilompatia Mtawala wa Ugiriki, Alexander Mkuu, maarufu Alexander The Great, wakati Greek ilipokuwa the 4th Super World hegemony kabla ya kifo chake.
Greek ilipoanguka baada ya kifo cha Alexander Mkuu na Warumi wakashika Dola, waliitumia 'idea' ya Aristotle, ya kutumia 'uchawi wa akili' (brainwash mentality) kuitawala Dunia kwa kuunda mfumo walioupa jina 'Roman Catholic' ambao baadae uligeuka kuwa dini na hatimaye kuzaliwa kwa kile leo tunaita Ukristo!
Ukristo (Urumi - Roman Catholic) ndio wahariri wa vitabu ambavyo leo tunaita Biblia!
Humo kuna siri nyingi na za ajabu.
Hiki kitabu ni coded book, kimejaa siri na mafumbo ambayo sio kila mmoja anaweza kuyafumbua mpaka mtu apitie kwenye shule maalum ya kuangaziwa (special enlightenment school) ambako 'codes' nyingi huvunjwa na vitu vingi kuwekwa waziwazi!

Naomba nisiendelee sana na hili, atakayetaka maelezo nitamweleza kwa kirefu kwa wakati wake.
Kuna 'gland lodges' ambazo ukiamua kwenda kusoma huko, kazi kubwa kwao ni kufungua akili yako na kuifunga upya, wanaondoa 'takataka' ulizoingiziwa kwa miaka yote uliyoishi duniani, unabaki kama ulivyozaliwa, unaanza upya. Hii tunaita 'mind reprogramming' (ni kwenye highest level of enlightenment, watoto wadogo hawaruhusiwi hata kupajua achilia mbali kupasogelea)

Sasa turudi kwenye point niliyosema huko juu kwamba mtu ni nyota na nyota ndiye mtu mwenyewe; na ya kwamba kabla HAJAZALIWA (ku-shift kutoka kwenye anga za mbali kuja duniani) 'ANAKUWEPO' na hata AKIFA (kuirudia asili yake, kule alikotoka) bado anakuwepo.

Namaanisha kabla wewe hapo hujakuwepo duniani, ULIKUWEPO na baada ya kuondoka duniani bado UTAENDELEA kuwepo.

Ushahidi wa vitabu vya kale unasema;

Numbers 24:15-17

"Akatunga MITHALI yake akasema, 'Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema,
Asema, yeye ASIKIAYE MANENO YA MUNGU, NA KUYAJUA MAARIFA YAKE ALIYE JUU. YEYE AONAYE MAONO YA MWENYEZI, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,

"NAMWONA, LAKINI SI SASA; NAMTAZAMA, LAKINI SI KARIBU; NYOTA ITATOKEA KATIKA YAKOBO NA FIMBO YA ENZI ITAINUKA KATIKA ISRAELI; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia."

Maneno "MITHALI" na "AONAYE MAONO" yaliyotumika hapo juu yanamaanisha;

MITHALI maana yake ni fumbo (parable)

AONAYE MAONO maana yake ni "the one who falls into terence" (tunamuita Clairvoyant - hii ipo kwenye mada ya Paranormal abilities, tutajifunza kwa mtakaokuwepo)

Huyo Clairvoyant (Muite Nabii au Mganga - Mwonaji au vyovyote utakavyo), aliweza kumuona MTU katika dimensions za juu na alimwita NYOTA!
Tunaanza kuelewana?

Hii Nyota ilikuja kuuvaa mwili (kuzaliwa duniani), miaka 600 baadaye!

Tusome maandiko;

Matthew 2:1-11

"YESU alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, MAMAJUSI WA MASHARIKI walifika Yerusalemu, wakisema,
Yuko wapi yeye aliyezaliwa, mfalme wa Wayahudi?
Kwa maana TULIIONA NYOTA yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.

Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?

Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.

Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.

Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ILE NYOTA WALIYOIONA MASHARIKI IKAWATANGULIA, hata ikaenda IKASIMAMA MAHALI ALIPOKUWA MTOTO.

Nao walipoiona ILE NYOTA, walifurahi furaha kubwa mno.

Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea TUNU; DHAHABU na UVUMBA na MANEMANE.
(HIZO TUNU; DHAHABU NA UVUMBA NA MANEMANE NI MASUALA YA MAFUSHO NA VITO/ MADINI YA NYOTA YA UTAWALA, NYOTA YA SIMBA - LEO SIGN, MTAJIFUNZA BAADAYE HUKO MBELE)

Nilichotaka muone ni MTU ambaye alikuwa HAJAZALIWA/ HAYUPO DUNIANI, lakini Clairvoyant aliweza kumuona.

Kuna Clairvoyants upande wa nyota, wanaweza kuona kila kitu kuhusu mtu ambaye atakuja kuzaliwa miaka ijayo. Wapo hadi leo.
Huyo Balaam Mwonaji alimwona Yesu, miaka karibu 600 kabla hajazaliwa, yaani HAKUWEPO!

Hao wanaoitwa mamajusi, yaani THE WISEMEN (wenye hekima) maarufu wataalam wa mambo ya Nyota, waonaji (Waite Wanajimu, Kiswahili cha kisasa), waliweza kumuona Yesu kupitia Nyota!
Hawa wataalam, ambao Biblia inawaita wenye hekima (the wisemen) walimwona Yesu kutokea umbali wa maelfu ya maili, yaani walikuwa Mesopotamia (Iran ya sasa) wakamwona kichanga aliyelala 'horini' huko Bethlehem (House of Bread - Nyumba ya Mikate) nchini Israel.

Sasa unaona kwamba MTU NI NYOTA NA NYOTA NDIYE MTU MWENYEWE!

Nyota inaonesha kiiila kitu kuhusu wewe.
Nyota yako inaonesha taarifa zako zote.
Mtu anayetaka kukutendea wema au ubaya, sio lazima awe karibu nawe, anaweza kukufanyia anachotaka kwa 'kuitazama nyota yako'!

Nina miaka zaidi ya 10 nikiwa 'mamajusi' (mtaalam wa kusoma nyota) hivyo najua ninachoongea kwa uzoefu wangu binafsi!

Zipo namna au njia nyingi za kusoma nyota ya mtu au kumwangalia mtu akiwa mbali au hata kabla hajazaliwa na ukajua mengi kuhusu yeye.
(Kwenye hili somo nitajaribu kufundisha baadhi ya hizo mbinu, nitafundisha kama 3 au 4 hivi, Asili ikiniruhusu)

Nimesema pia huko juu kwamba hata unapoondoka duniani (UNAPOKUFA) bado unaendelea 'ku-exist' (kuishi) ila sio kwenye dimensions hizi za chini, bali huko nyanda za juu na watu wenye uwezo wa Clairvoyance (waonaji - clairvoyants), wanaweza kukuona wakitaka.

Angalia mfano;

Matthew 17:1-3

"Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani;
akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Na tazama, WAKATOKEWA NA MUSA NA ELIYA, wakizungumza naye"

Hao waliotokea kwenye terence kule mlimani, Eliya na Musa, ni watu walioishi miaka mingi sana huko nyuma na walishaondoka!

Walienda wapi?

Huko walikokuwa wametoka mwanzoni!

Wapi?

Kwenye ulimwengu wa roho au ulimwengu wa Nyota!

Kwa hiyo pale hawakutokea physically, bali spiritually au astrologically, namaanisha kinyota!
Wale walioonekana, Musa na Eliya, hawakuwa katika miili ya damu na nyama, zilikuwa nyota zao na ndio maana walionekana wakati waliowaona walikuwa kwenye terence state!

Itoshe kusema kwamba WEWE NI NYOTA kabla hujazaliwa na utaendelea kuwa Nyota hata ukifa!

Kinachofanyika pale wazazi wako 'wanapolalana' ni kukuumba kimwili (kukupa mwili) tu.
Wewe sio huo mwili, wewe ni Nyota fulani!

Je, waijua nyota yako ambayo ndio wewe mwenyewe?
Au niseme unajijua wewe ni nani?
Wajua mengi au yote kuhusu nyota yako, ambayo ndio wewe mwenyewe?

Utajua kila kitu hapa hapa kwenye Enlightenment Class 2.

Sit, Watch, Relax!

Mambo mazuri yanakuja.

Dr. Rwakiunge Rugambwa (PhD),
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho.
 
Huyu ananyota hifadhi ya gombe kigoma

IMG_0612.jpeg
 
Back
Top Bottom