Nyota njema ilianza kuonekana mapema kwa rafiki yangu

Ila haya maisha usimdharau mtu sio usiemjua tu "NO" Usimdharau mtu yeyote yule, penda kuishi na watu vizuri bila kuwafanyia/kuwatendea ubaya.

Huyu mwamba alikuwa classmate tulikuwa na ukaribu kiasi fulani na mawasiliano kiasi, alikuwa bangi sana ila yupo real. Ni miongoni mwa waliokuwa wanadharaulika sana class kutokana na muonekano wake ila sikuwahi mdharau kwa chochote.

Kwa niliosoma nao yeye pekee ndie mwenye uwezo zaidi, tumepotezana kwa miaka, mwaka jana mwishoni alinitafuta kunipa dili fulani litakaloninufaisha likitamatika, kwa bahati mbaya sikuwa kwenye mazingira ya kukamilisha dili na nikamwambia na jibu likawa moja tu ukiwa tayari we niambie nimekupa hili dili kwakuwa hunaga madharau na unaheshimu kila mtu. Jana kanicheki tena inshallah kesho pakikucha salama nitaonana nae tuendelee na jambo letu la faida.
 
Kuna watu watajua hii ni kwel eti
Arusha miaka ya 80 kuna mtu alikuwa anaitwa Virani...Tango transport.....watoto wake wanapomaliza std 7....aliwazawadia magari mapya ya dukani km.0..Peugeot 505....one ten....range rover.....na binti yake toka Arusha school alipewa Mercedes Benz...kama ya Rais wakati ule.
 
Shukran sana 🫡🤝
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…