Nyota wa Yanga Kibwana Shomari, Dickson Job na Abuutwaleeb Mshery kutoa msaada wa bima za afya kwa watu 500 Morogoro

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Nyota wa Yanga, Kibwana Shomari, Dickson Job na Abuutwaleeb Mshery wamepanga kutoa msaada wa bima za afya kwa watu 500 mkoani Morogoro kupitia tamasha lao la Wape Tabasamu 2025

Kilele cha tamasha hilo ni Jumapili, Julai 6, 2025 ambapo kutakuwa na mchezo baina ya timu zinazoongozwa na wachezaji hao

Mwenyekiti wa Tamasha la Wape Tabasamu, George Job ambaye ni meneja wa wachezaji hao amesema kuwa kundi la watakaonufaika na bima hiyo ni Wazee na Watoto

“Jambo kubwa ambalo tumepanga kulifanya mwaka huu ni kuchangia huduma ya bima ya afya kwa watu 500. Na hili kutimiza hilo tunahitaji kiasi cha Sh66 milioni kwa ajili ya bima za afya kwa watoto 250

“Na kunahitajika kiasi cha Sh177 milioni kwa ajili ya bima za afya kwa Wazee. Kingine pia tumepanga kutoa mafuta kwa maofisa usafirishaji au bodaboda,” amesema Job

Beki Kibwana Shomari amewataja baadhi ya nyota wa timu yake ambao watacheza mechi hiyo

“Upande wa timu yangu kutakuwa na Maxi Nzengeli, Saimon Msuva, Mbwana Samatta na wengineo ambao mtawaona pale uwanjani,” amesema Kibwana

Kwa upande wa Dickson Job, amewataja Pacome Zouzoua, Abdulrazack Hamza na Aziz Ki kuwa miongoni mwa nyota watakaocheza mechi hiyo kwa upande wa timu yake

​
 
Kweli Rage hakukosea, hizo bima hazina ubaguzi watapata mashabiki wa Simba ,yanga na timu zingine pamoja na wale ambao hawana ushabiki kwa timu yeyote Ile.
Achana nae huyo mtoto wa shule hawezi kua na hela zaidi ya mavi tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…