Nyota wanne wa Yanga kuikosa mechi ya Weaita Ditca ya Ethiopoia leo

Nyota wanne wa Yanga kuikosa mechi ya Weaita Ditca ya Ethiopoia leo

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga itarajiwa kushuka dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam mnamo Aprili 07, 2018 kuwavaa Welaita Ditcha ya Ethiopia huku ikiwakosa nyota wake wanne kutokana na kuwa na kadi za njano.
Wachezaji hao ni pamoja na Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Said Juma Makapu na Kelvin Yondani.

Yanga Logo.jpg


Hayo yamebainishwa na wachambuzi wa soka kutoka tinga namba moja kwa vijana EATV asubuhi ya leo na kusema kwa mujibu wa sheria za CAF mchezaji yeyote akipata kadi mbili za njano kwenye mechi za kimataifa basi mchezo unaofuata hatoweza kushiriki kwa namna yeyote ile.

Yanga itahitajika kupata ushindi katika mchezo huo ili waweze kujikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia katika hatua inayofuata ya makundi katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho.

Chanzo: EATV
 
Poleni watani zangu.Chirwa angeamua matokeo.Wajengeni kisaikolojia vijana kama vile Maka, Yusuf Mhilu na wengineo.
 
Utulivu huu ni kwa hisani ya Singida United..!
 
Watajua wenyewe...wameniudhi sana juzi
Bado mnashabikiaga Simba na Yanga? Subirini mje mwone maajabu ya Simba kwenye hizi mechi za mwisho mwisho, ndicho kipindi huwa wanalilia pointi za mezani!
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] nilitamani nione jinsi ulivyokua unaandka haya maneno. Nimecheka mno
Acha tu mkuu...naona msimu ujao hatupandi ndege
 
Hao ndo nyota?mnachekesha sana
 
yanga bhana...pamoja na kuwepo hao "nyota" kwenye mechi yenu juzi bado mlikalishwa....sasa je bila hao nyota?
 
Nipo Upande wa Ditcha fc ya Ethiopia!
 
Tushapigwa duuu sijui nani alituloga sisi wakimataifa
 
Back
Top Bottom