real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga itarajiwa kushuka dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam mnamo Aprili 07, 2018 kuwavaa Welaita Ditcha ya Ethiopia huku ikiwakosa nyota wake wanne kutokana na kuwa na kadi za njano.
Wachezaji hao ni pamoja na Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Said Juma Makapu na Kelvin Yondani.
Hayo yamebainishwa na wachambuzi wa soka kutoka tinga namba moja kwa vijana EATV asubuhi ya leo na kusema kwa mujibu wa sheria za CAF mchezaji yeyote akipata kadi mbili za njano kwenye mechi za kimataifa basi mchezo unaofuata hatoweza kushiriki kwa namna yeyote ile.
Yanga itahitajika kupata ushindi katika mchezo huo ili waweze kujikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia katika hatua inayofuata ya makundi katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho.
Chanzo: EATV