Nyota ya Magharibi yang'aa, mbegu yachipua, Kitoto Chaanza Tambaa!

Zakumi,

Kwa sasa hivi sipigi baragumu la Ideology bali ni kuhusu Principle ambazo tunazo ambazo zimepuuziwa. Si suala la CHADEMA versus CCM au CUF versus CCM, bali it is about Doing Right things versus doing wrong things.

Tanzania tunahitaji tubadilishe attitude, na hili ni Taifa zima na si CCM pekee. Zitto kato wito kwa Watanzania kubadilisha mazoea na kuanza khoji vitu.

Hata kama CHADEMA au CUF wakiingia madarakani na Watanzania wakaendeleza libeneke kama tuliloliendeleza na CCM< hatutapata maendeleo kupitia falsafa ya Ubepari au Soko Huria.

Kukwama kwa Tanzania kwenye tope si kuhusu Itikadi au Sera, bali ni kukosekana kwa mwamko wa kufanya lile lililo sahihi.

Angalia Mizengo Pinda analia kuwa Uongozi ni mbaya na dhaifu, yeye ndiye mkuu, na badala ya kubadilisha mwelekeo ili kuwajibisha watu wawe wachapa kazi, anaishia kulalamika kama sisi Wananchi.

Angalia Kikwete, analia hajui chimbuko la umasikini wetu, kama Rais wa nchi, lakini hajafanya lolote la mwamko kuamsha mbegu mpya ya kutaka uwajibikaji.

Swala sasa hivi si Ujamaa au Ubepari, bali ni kufuata sheria, kanuni, maadili, kuwajibika na ufanisi.
 
nimekuwa nikitamani sana hii elimu ninayo ipata hapa inanifungua macho naona mbele tunako elekea,nabaki na swali kichwani mwangu je hao ndugu zangu huko vijijini wataipataje hii elimu kama mimi ninavyo ipata? naungana na wewe kwamba kama ikiwezekana JF tutoe chapicho letu ambalo tutaligawa bure wananchi,nipo tayari kuchangia gharama kwakutoa lakimbili huu ni mwanzo tu.Kama mtakubaliana na ombi ili tafadhali sana tutafutane tukutane then tujadiliane kwa kina. Invisible,Shy,Haika,na wengineo mnasemaje kuhusu hili jambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…