Nyufa katika madirisha

Kitumburee

Senior Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
142
Reaction score
88
Poleni na majukumu wakuu.

Nimejenga nyumba yangu iko ktk hatua ya kupaua ila nimeona katika madirisha matatu kumetokea (nyufa nyembamba sana) unakua ni ufa mmoja tu unata juu mwenda chini.

Fundi anasema ni kawaida nyufa kutokea madirishani na zitarekebishwa wakati wa kupiga llaster, je kuna ukweli wowote?
 
Ndiyo ukweli upo, wakati najenga kibanda changu kimoja ilitokea,baadaye fundi wa plasta aliweka wire mesh in miaka 6 sasa haijatokea crack
 
Wakati wa kupiga kenchi uliweka ubao juu ya ukuta kuzunguka jengo lote yaani wall plate? Au uliweka vipisi vipisi kenchi inamokalia?

Kama uliweka vipisi Basi hiyo ndio sababu unakuwa umesababisha point load badala ya kufanya uniformly distribution load
 
Inatokana na kutanuka na kusinyaa kwa mbao (Kama umeweka dirisha za mbao)

Haina shida kabisa hii kreki.

Ziba na wayameshi Kisha piga rangi Kama kawaida
 
tuma picha ya kibanda chako! isije ikawa ni fundi maikoo..! ushaharibu unajaribu kusoma kwetu urekebishe..😁😄
 
Nadhani uneongea kiufundi na hii ndio point .nasoma comment yako nikaangalia juu nikaona kweli fundi hakupiga mbao kuzunguka jengo.na hii creck ninayo kwenye dirisha 3.nilishapiga hiyo wire mesh wakati wa plaster Ila naona Kwa mbaaali zimerudi
 
Thanks mkuu. Sasa ukipiga plasta hapo huo uwazi si utaonekana kama ufa? Au wire mesh ikitumika inasolve hilo?

Ndio maana kwenye ujenzi wanashauri ufuate steps za ujenzi ,ukishajenga unaiacha kwa muda ititie na kujiweka sawa,wakati inajiweka sawa ndio hizo expansion joint zinasaidia kutotokea kwa nyufa,nyumba ikishatulia ikisha kuwa stable hata ukipiga plasta hakuna shida.
 
Nmekupata mkuu. Asante kwa ufafanuzi
 
Nawashukuruni nyote kwa inputs zenu. Hapo itabidi nitumie wayemesh
 
Sijawahi ona hii, embu tupia picha kama tz inafanyika hii.

Mbona zingine haziwekewi ubao, na hazipasuki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…