Jesusfreak08
JF-Expert Member
- Jul 20, 2019
- 822
- 1,803
Kuna mtazamo wa watu wengi sana kuhusiana na nyuki lakini kwa kifupi nataka tujifunze mambo machache kuhusu hawa wadudu na umuhimu wao sana katika muendelezo wa jamii ya mimea mbali mbali
Nikuibie siri tu ni kweli nyuki wanazalisha asali lakini kuna kitu kikubwa sana wanakifanya kwa mimea inayotoa maua kwa tukitolea mfano wa maparachichi au alizeti ni miongoni mwa mimea ambayo inategemea sana hawa wadudu
Ukitaka kupata parachichi au alizeti zenye ubora basi hakikisha hawa wadudu wanakuwa karibu na shamba lako kwasababu wanasaidia sana katika uchavushaji wa matunda katika mimea hii
Ukiangalia mmea kama alizeti zaidi ya asilimia 87(87%) inategemea sana katika uchavushaji kwaiyo kama shamba lako la alizeti litakosa mizinga ya nyuki basi ni uhakika utapa mavuno machache sana
Na hivyo hivyo kwenye maparachichi ni jambo hilo hilo unaweza usipate Matunda
Kwaiyo sasa tambua leo nyuki sio kwaajili ya asali tu bali wanaumuhimu sana katika mazao yetu hasa inayotegemea uchavushaji
Watu wengi tumezoea kupiga dawa kwenye mashamba yetu tunasahau upigaji dawa unaathiri hata wadudu hawa ambao wana umuhimu na inapelekea ukosefu wa mazao kwa wingi ili kuweza kuzuia tatizo hili hakikisha unapiga dawa kabla ya mmea wako kutoa maua ni muhimu sana sana
—Tushiriki kuwalinda wadudu hawa kwa faida yetu wenyewe