Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
NYUMA YA MTAALA WA ELIMU WA TANZANIA
Naomba nianze na ile salamu yetu ya " Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee".
Leo tarehe 6/4/2021 nimefarijika sana baada ya kusikia kauli muhimu " tendo uneni" kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Samia Suluhu Hassan ikihitaji mtaala wetu kuangaliwa kwa jicho pevu.
Kauli hii muhimu katika mustakabali wa elimu Nchini imelenga kusukuma tathmini ya elimu ili kupata elimu bora itakayonmsaidia Mtanzania kuliko hali ilivyo sasa. Hali hii inaonesha kuna tatizo kubwa katika elimu yetu. Sharti tujiulize huu mtaala uliopo kwa nini upo ulivyo na kwa nini unazalisha wasomi wa aina tunayoiona Nchini.
Serikali mekuwa ikitatua kero nyingi zinazohusiana na elimu mara kadhaa kwa kuuangalia mtaala wa elimu na kuacha suala linaloutawala mtaala wa elimu yaani "Falsafa ya Taifa". Huu ndiyo wakati muhimu wa kuiangalia falsafa yetu kwa makini zaidi kama tunataka kufanya kuhakikisha elimu itasaidia kila Mtanzania.
Kabla ya kuangalia Mtaala sharti tufahamu kwa dhati kabisa "TUNATAKA KUJENGA TAIFA LA NAMNA GANI?.Kama hatufahamu aina ya Taifa tunalolitaka ni vigumu sana kupata suluhu ya kudumu ya changamoto na matatizo ya elimu yetu.
Tukifahamu barabara aina ya Taifa tunalotaka kilijenga ndipo tutakapoweza kuweka mipango ya elimu yenye kufikisha kwenye shabana hiyo (Nyerere, 1968). Ipo kila sababu ya shabana na nguzo za Taifa kuwekwa wazi na kueleweka kwa kila mtu. Kwa mfano falsafa ya ujamaa kama ilivyoasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius. Kambarage Nyerere ilitamka wazi nguzo tatu ambazo ni;
(i) Usawa na heshima za ubinadamu
(ii)Kushirikiana mali inayotokana na juhudi zetu
(iii)Kazi kwa kila mtu na kufuta unyonuaji.Mambo haya matatu yalielekezwa kuwa ni Kanuni za Taifa. Tunapoona shida kwenye elimu yetu tunapaswa kuangalia Kanuni zetu zinasemaje?.. Je tunazifahamu kwa dhati kanuni za Taifa letu?.
Elimu yetu imekuwa ikisukumwa sana na kumbo la wakati na mahitaji yake kuliko mahitaji halisi ya jamii yetu " SHABAHA YETU". Utandawazi umesababisha mabadiliko makubwa kwenye mtaala wetu wa elimu kuliko namna ambavyo mtaala wetu ulipaswa kuendana na shabaha yetu "AINA YA TAIFA TUNAOLIHITAJI".
Watanzania hatuna budi kukubali hali ya elimu ndani na nje ya Nchi yetu ilivyo sasa lakini "TUNALO JUKUMU LA KUHAKIKSHA HALI HIYO INAENDANA NA SHABAHA YETU. Kwa maana nyingine ni kwamba, pamoja na kupokea mabadiliko makubwa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaosukumwa nautandawazi bado tunapaswa kuangalia shabaha yetu " AINA YA TAIFA TUNALOLITAKA"
Tunaweza tukaingia katika utandawazi ila badala kuiga kila kitu tukachanganya "glocalization" bila kutoka kwenye shabaha. Nchi kama Japan inaonekana kufanya vizuri kwenye teknolojia na pia elimu kwa kutokana na tabia ya kuchukua na kuchanganganya na utamaduni wake. Hali hii inalifanya Taifa kulinda shabaha yake.
Mambo haya yote yanahitaji zaidi ya matamko ila yanajikita zaidi katika utendaji wa ila siku imani ya jamii. Tunapaswa kufikia mahali ambapo kila Mtanzania anakuwa siyo tu sehemu ya utekelezaji ila utekelezaji wenyewe wa shabaha ya Taifa hili.