Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Nafuatilia kinamna siasa za nchi hii. Ni siasa za kihuni sana. Siasa ambazo wanasiasa wanaamini hawawezi kuishi bila siasa.
Hawawezi kuishi bila kuwa chama tawala. Hawawezi kujitegemea bila Dola na viambatanishi vyake.
Ni siasa za kukereketa, hasa ukiwa nje ya chama tawala. Ni siasa za kufa na kupona. Kumbe kuna maisha baada ya siasa.
Kwa upande wa pili siwalaumu sana upinzaani kutokana na mazingira niliyoeleza hapo juu. Wapo watu na huwa sijui huwa wanatoa wapi uthubutu huo wa kukosoa, na ukiwafuatilia wala sio wanasiasa.
Wiki hii na iliyopita zilikuwa ni wiki za CHADEMA. Tumeshuhudia chama kwa umoja wake kikifanya press/mkutano na kuzungumza yanayohusu chama na mustakabali wake wa kisiasa kuelekea 2025. Hatujapo, M/Mwenyekiti mzee Lissu naye akasema ataitisha press. Na kweli kaitisha na kaongea haswa. Kwamba naye sasa anautaka uenyekiti. Aliongea bila kupepesa.
Tukio hilo limanirejesha nyuma kidogo kwa habari ya Dr. Slaa. Baada ya Lowasa ((RIP) kukaribishwa chamani kwa lengo la kugombea urais kupitia CHADEMA, jambo hilo halikumfurahisha Dr. Slaa. Naye aliitisha press na kutema nyongo. Tulidhani ni mbinu za kisiasa dhidi ya CCM kumbe mzee alikuwa serious. Baadaye akakibwaga chama na kuungana na watesi. Babati nzuri chama kiliendelea kuwa imara japo misukosuko ilikuwa mingi.
Zikapita nyakati ukaja uchaguzi wa wenyeviti w kanda CHADEMA. Palipokuwa pagumu na penye mvuto palikuwa kanda ya Nyasa ambapo Sugu na Msigwa walikuwa wanawania nafasi hiyo.
Mdahalo ule kati ya wagombea niliuona kupitia Star Tv. Kiukweli wale wagombea walikuwa serious sana. Kadhalika kwa manibizano.yale japo wakati mwingine yalijaa ukakasi, sikutaka kuamini kwamba walimaanisha. Nilijua ni mbinu za kichama na kutanuka kwa demokrasia. Kwamba wanaionyesha CCM kuwa wao wanajibizana kwa hoja na hakuna kuogopana.
Uchaguzi ukapita na Msigwa akabwagwa. Naye akasema ataitisha press. Nikajua tena ni mikakati ya kichama, ila haikuwa hivyo. Baadae akakimwaga chama na kuungana na watesi. Bado chama kiliendelea kuwa imara.
Leo tena historia inaendelea kujirudia. Chama kimejaa fukuto. Nafasi ya uenyekiti inawaniwa na Lissu na bila shaka Mbowe. Lissu anazungumza bila kupepesa.
Anamsema Mwenyekiti bila kificho. Bado natamani kuamini kuwa ni mbinu na mikakati ya kichama dhidi ya CCM. Bado nataka kuendelea kuamini kuwa Lissu na Mbowe wako imara.
Wana ajenda dhidi ya CCM.
Tunasubiri uchaguzi ufanyike, tupate na matokeo. Na matokeo yawe ya amani. Tunajua pia kuwa CCM inahaha kila kona. Inshambulia hadharani na faraghani kuona tu, CHADEMA inakufa. Inasambaratika.
Kama ni mkakati wa kichama, na uwe wenye heri. Wapo walioanza kwa staili hiyo ila waliponogewa wakamaanisha kweli. Wakasaliti mikakati na kutokomea.
Lissu bila shaka sio wa hivyo. Naona kama wasemavyo wengine kuwa chama kinaenda kumeguka mapande mawili. Ili iweje? Kumfurahisha nani? CCM? Hapana.
Ikibidi, uchaguzi huu wa nafasi ya uenyekiti ufanyike kwa staha sana na uwazi sana na bila mizengwe. Atakyeshinda na ashinde kwa haki.kabisa.
Naamini safari hii historia haitajirudia. Hatatoka mtu kwenda kuungana tena na watesi. Tunaitamani Tanzania mpya