Nyumba aina ya Contemporary ni mchongo

Ijagara

Member
Joined
Dec 15, 2021
Posts
29
Reaction score
64
Habari zenu wana JamiiForums,

Napenda kuwa fahamisha kuhusu nyumba Aina ya contemporary ( nyumba za bati za kuficha). Nyumba hizi huwa na muonekano mzuri sana kama utapata mtaalam mzuri wa kukuandilia ramani nzuri yenye kukidhi vigezo vyote vya kitaalam.

Ni Aina ya nyumba zinapendwa sana Katika zama hizi. Mathalani, waliovijana hupendelea sana kujenga nyumba za Aina hii.

Lakini pia, nyumba hizi huwa complicated sana kwenye ujenzi hivyo, huhitaji kuwa na mtaalam (engineer au architect) Katika kipindi Cha ujenzi au fundi mzoefu na mbobezi anaeweza kusoma na kutafsiri vizuri ramani ya kitaalam.

Chini ni picha za nyumba Aina ya contemporary yenye 1 master bedroom, chumba Cha kawaida kimoja, store, public toilet, open kitchen, sitting room na dinning ndogo, ikiwa pamoja na varanda kubwa ya mbele na ya nyuma.

LOCATION: BURONGE, KIGOMA.

NYUMBA IMEJENGWA KWA USIMAMIZI WA KITAALAM.

NAOMBA KUWASILISHA.View attachment 2046663View attachment 2046664View attachment 2046665
 
Kontemporary inabidi iinuke juu sana kama ya chini ila kwa ghorofa ndiyo zinapendeza sana.
 
Razima tuambizane ukweri ndugu zangu Watanzania Contemporary au bati la kuficha ni za sehemu kama Dubai ambapo mvua hazinyeshi mara kwa mara huku kwetu zitasumbua tu ni issue ya muda
Sio kweli,contemporary zilikuwepo tangu zaman,tatizo mafundi wengi hawajui kuzijenga hasa upande wa roofing wengi hajui kupaua,Pili zinahitaji close supervision na sio kuachia mafundi ili kukwepa gharama za kulipa Architect au Engineer.
 
Hizi nyumba nimeshindwa kuzielewa kabisa.
Hata ikiwa imekamilika naiona kama nyumba nusu ambayo haijaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…