Habari wadau,nilipita eneo flani hapa dar nikasikia vijana wakibishana,upande mmoja ulikua unasema ukipata pesa afadhali ufanye biashara kwanza ndo baadae biashara ije ikupe makazi,yaani ujenge nyumba yako ya kuishi na upande wa pili ulikua unasema bora nyumba kwanza halafu ndo uje ufanye biashara sasa wewe mwenye ndoto za kuwa mjasiriamali siku moja unadhani kipi ni bora?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mimi naona Kwanza unatakiwa Ufanye Biashara, nyumba mara nyingi kama ni ya Kuishi haina return so huwezi kuila hiyo nyumba, ila ukiwa Mjasirimali na ukafanikiwa kujenga ni simple sana tena sio kujenga unanunua gheto likiwa na kila kitu wewe ni kwenda na Nguo zako tu kuanza maisha,
Kweli kabisa mkuu chasha,ile kuambiana kwamba ukipata pesa jenga kwanza haina nguvu asilimia mia kwa mtu anayesaka uhuru.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Inategemea, kama muajiriwa jenga kwanza pale ulipo. Ukihama waweza uza nyumba na kupata mtaji. Kumbuka ulijenga kwa pesa za kudunduliza, ukaishi kwenye hiyo nyumba na ukiuza unapata pesa ya pamoja ambayo yaweza kuwa mtaji wa biashara.
Mkuu watu wanatofautiana malengo na mataji wa biashara maana hapa mtoa mada hajazungumzia mtaji wa kiasi au nyumba ya sh ngapi, kuna mtu mwingine anaweza jenga ili apate sifa ya kuwa hadhi ya kupata hela nyingi hata kwenye mabenki ili afanye biashara kubwa hii inatokana na kipato chake cha awali kuwa kidogo kidogo alishindwa kufanya biashara.Maisha hayana kanuniMimi naona Kwanza unatakiwa Ufanye Biashara, nyumba mara nyingi kama ni ya Kuishi haina return so huwezi kuila hiyo nyumba, ila ukiwa Mjasirimali na ukafanikiwa kujenga ni simple sana tena sio kujenga unanunua gheto likiwa na kila kitu wewe ni kwenda na Nguo zako tu kuanza maisha,
Mkuu sijajua unazungumzia nyumba ya thamani gani na wapi maana ukiwa na uwezo wa kununua nyumba nzuri kwa cash sidhani hata mjadala huu unakuhusu kwa maana nyingine mambo safi hasa kwa maisha ya wa TZ wengiNi kweli haa Mambo ya Kujenga yapo tu na ni pesa yako, siku hizi watu kwanza hawataki kujihangaisha na mafundi, mtu anafika na kununua kitu ikiwa tiyali,
Ujue katika maswala ya Kiuchumi kujenga Nyumba kwa pesa yako mwenyewe ni makosa sana, ila Ndo kama hivyo na mara nyingi nyumba za kuishi inatakiwa zijengw kwa mikopo ya Muda Mrefu kwa sababu haina return kabisa
Jenga nyumba halafu chukulia mkopo ufanyie biashara ukiona mtaji unataka kuzama unafunga biashara unarudisha mkopo fasta unabaki na nyumba yako. Kesho ukipata biashara poa zaidi unachukua tena mkopo nyumba iko palepale. Mambo ya kusema usijenge ufanyie biashara uwezekano wa mtaji kudidimia na biashara kufa ni mkubwa kwa kuwa hakuna mabiashara yenye uhakika wa kuleta faida wakati wote na kama yapo yalishakamatwa na wajanja kitambo sana.
Pessmistic.....unavyosema hakuna hata kama ipo umeshaufunga ubongo wako kuona fulsa....tatzo la umaskin sio fulsa wala mtaji ni the way maskini anavyofikili,ndo maana matajili ni wa chache cz n wa2 wachache waliokubali kuwaza tofauti...
Wewe ni tajiri? kiingereza kibovu, kiswahili kibovu utaelewekaje? si bora unyamaze au ongea basi kikwenu. Kwa ubongo wako wewe unaouona supa kila anayeanzisha biashara anapata faida na kutajirika? Unajua kitu trial and error? kwanini vyuoni wanafundisha probability? acha kuongea pumba kwanza hueleweki
usiwake kaka..kubali changamoto ya kubadilika,ni kweli co mzuri kwenye both kiingereza na kiswahili lakin tofauti ni the way 2navyofikili 2....nafasi zipo ni kufikili kwako 2,nakuacha na this two quotes utafakali kwa makini kabla hujawaka tena cz i know ua a gr8t thinker ndo maana upo humu ndani...1.As a man thinketh in his heart, so is he.... 2.Whether you think you can, or you think you can't--
you're right .