Nyumba imejengwa juu ya kaburi la Abushiri bin Salim al Harith

Kwahiyo African Association kilikuwa chama cha kidini cha waislamu kama Muslim brotherhood cha Masri?
 
Mkwawa alikuwa na urafiki mkubwa na Waarabu na alikuwa akifanya nao biashara ya pembe za ndovu na wao waarabu ndio waliompa bunduki Mkwawa kwa mara ya Kwanza.

Na hata mavazi asili ya wahehe ya kuvaa mashuka meupe ni Mkwawa ndio aliletewa hayo mashuka na Waarabu na ndio limekuwa vazi lao la asili kama unavyoona Wamasai.

Ni kweli Mkwawa aliingia kwenye uislamu kwa sababu Waarabu ndio walikuwa washkaji zake na hapakuwa na dini kwenye nchi ya uhehe.
 
Nashauri wasomi watafsiri hivi vitabu likiwemo hiko kilichoonyeshwa kiwe katika lugha ya Kiswahili kitasaidia vijana wetu kuvisoma na kivielewa.Ni ushauri tu sio lazima
 
Kwahiyo alikua Dalali?
 
Wyatt,
Hili ndilo tatizo kubwa linalokabili historia ya uhuru wa Tanganyika na historia yake Nyerere.

Wanaona tabu kueleza ukweli na ikafanyika juhudi kubwa ya kuififilisha historia ya kweli.
 
Kwahiyo alikua Dalali?
Sijui nimuite vipi, ila mbuga ya Ruaha ipo Iringa, na yeye ndio alikuwa mtawala wa nchi ya Uhehe, kwahiyo alikuwa akitumia rasilimali zao za Uhehe kuwauzia Waarabu.

Walikuwa wakifanya bata trade zaidi kuliko pesa.
 
Hivi waarabu hawajafanya biashara ya utumwa

Ova
Hujasikia Waafrika walifanya biashara ya watumwa? Biashara huwa na pande mbili: anayeuza na anayenunua. Pamoja ya yule anayezalisha bidhaa.
Kwa jumla Waafrika walizalisha bidhaa yaani watumwa kwa kukamata wafungwa, halafu kuwauza. Waarabu walikuwa wateja wakubwa, hasa katika biashara ya kuwapeleka ng'ambo;
tangu Waingereza walibadilika kutoka wafanyabiashara wakuu wa watumwa kuwa wapinga biashara hiyo, waliwasumbua Waarabu karika Afrika ya Mashariki hivyo walianza kutumia watumwa wengi kwa kazi kwenye mashamba waliyoanzisha pwani na Unguja.

Kwa hiyo: unataka kusema nini Waarabu walifanya biashara ya watumwa? Nisipokosei watu wa pekee ambao hawakufanya biashara ya watumwa walikuwa Maasai.
 
Hamza mwengine...!
Geza...
Sijui una maana gani kusema "kulalamika."

Ikiwa historia iliyoandikwa si kweli akatokea mtu akasahihisha kama nilivyofanya huku ni kulalamika?

Wataalamu wanakichukulia kitabu changu kama "corrective history."

Wewe umetoa maoni yako unasema naandika "dini," je huku ni kulalamika au ni kueleza fikra zako?

Mimi nimefanya utafiti katika historia ya Waislam kutaka kujua kwa nini wao walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na Wajerumani na pia Waingereza na kwa nini Wengine walikuwa nyuma.

Nikaenda mbele zaidi kutaka kujua kwa nini baada ya Tanganyika kukombolewa kukazuka matatizo ya ubaguzi dhidi ya Waislam?

Hii ni "field of enquiry," mfano ambao wasomi kote ulimwenguni hufanya ili kujua tatizo liko wapi na kutafuta ufumbuzi wake.
 
sasa usalama wa huyo Mholanzi aliyeuziwa kiwanja na serikali unakaaje? Yeye kama hakujua anahukumiwa vp? Huoni maandishi yako yana chembe ya kujenga chuki? halafu tafiti zako ni historia ya Waislam tu? Mbona Mkwawa alikuwa Muislam wenzio walifanya tafiti na hawakulenga kum-categorize kwenye Uislam bali kama chief aliyepigania maslahi ya wananchi wake?
 
sasa usalama wa huyo Mholanzi aliyeuziwa kiwanja na serikali unakaaje? Yeye kama hakujua anahukumiwa vp? Huoni maandishi yako yana chembe ya kujenga chuki?
Geza...
Hapana tatizo lolote kuhusu utafiti wa historia ya Abushiri.

Nimefika Pangani zaidi ya miaka 100 baada ya Abushiri kunyongwa na watu wanaizungumza historia hii kama wanavyoeleza historia nzima ya wazee wao na Wajerumani.

Sikupata kusikia lolote la kuashiria chuki au mfano wa hayo.

Kuhusu "categorisation," hili ni suala binafsi la mtafiti kipi anataka kutafiti.

Naona unataabishwa sana na historia ya mapambano dhidi ya dhulma za wakoloni kuhusishwa na Waislam.

Hauko peke yako.

Laiti nisingeandika kitabu cha Abdul Sykes historia nzima ya TANU ingebebwa na Nyerere peke yake.

Wote wazalendo waliokuwa katika kupigania uhuru wangetoweka.

Tusingekuwa na historia ya kweli.
 
Mzee, ukiuliza maswali kuhusu ubaguzi wa waislamu katika Tanganyika unauliza maswali yenye maana.
Ila sijui itasaidia nini ukipinda historia ya Waislamu na ukoloni?
*Ni kweli kwamba Waislamu walipatikana kwenye mstari wa mbele wa kupinga mwanzo wa ukoloni wa Wajerumani. Umetaja mifano
`*Ni kweli pia kwamba uvamizi wa kikoloni katika Tanganyika ulitekelezwa na wanajeshi Waislamu chini ya maafisa Wajerumani. Maana jeshi la kijerumani la Schutztruppe lilianzishwa hasa na askari mamluki kutoka Nubia (Misri kusini / Sudani kaskazini) na hao "Wasudani" walikuwa uti wa mgongo wa jeshi la "Kijerumani" kwa miaka mingi. (lilipoanzishwa 1888 na Wissmann lilikuwa na maafisa 21 na masajini 40 kutoka Ujerumani, askari mamluki Wasudan 600 walioongezwa na Wazulu 150 kutoka Msumbiji)
*Ni kweli kwamba utawala wa kikoloni ulitegemea Waislamu waliojua kuandika na kusoma; Wajerumani walikuwa wachache mno; walipompata chifu aliyeweza kushirikiana nao, walimtumia chifu kwa kusimamia eneo. Pale ambako hawakukuta machifu, waliweka maakida waliosimamia maeneo ya vijiji kadhaa. Siwezi kukumbuka kutoka miaka ya kwanza hata akida mmoja ambaye hakuwa Mwislamu. Ukali wa maakida ulikuwa sababu muhimu ya Wamatumbi kujiunga na harakati ya Kinjitikile na kuanzisha vita ya maji maji; akida wa kwanza aliyeshambuliwa na wanamajimaji aliitwa Sefu bin Amri.
* Wamisionari Wajerumani walilalamika mara kwa mara kwamba jeshi la kikoloni lilisambaza Usilamu kote Tanganyika. Maana kwa wenyeji wengi uso wa utawala wa kikoloni haukuwa yule Mjerumani mmoja aliyekaa mbali nao kwenye boma lake (vituo vichache nchini), lakini askari wa kikoloni aliyepita katika vijiji vyao ambaye alikuwa mara nyingi Mwislamu;
*umefanya utafiti kuhusu historia ya akina Sykes; ukiuliza kwa nini mamluki Mzulu anageukia Uislamu jibu mojawapo ni kwamba alikuta askari wenzake wenye vyeo na heshima katika jeshi la kikoloni walikuwa Waislamu, sivyo? Aliendelea kwa uhodari kueneza utawala wa Kijerumani kote alipotumwa - na pia kueneza dini yake.

Sitaki sasa kugeuza masimulizi yako kinyume, au kuwashtaki Waislamu.... Lakini historia halisi ina nyuso nyingi. Kuteua yale tu ambayo mimi au wewe tunapenda haileti picha ya kweli.
 
Mwana...
Nakushukuru kwa mchango wako.
Ikiwa niliyoandika mimi si ya ukweli ukweli ni upi?
 
Pitia hiki kitabu ili uipate Historia mujarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…