Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mzee Said na familia yake nje ya nyumba yake na. 81 Mtaa wa Aggrey
Picha hii imepigwa 1955
Picha hii kaniletea rafiki yangu toka utoto Juma Khube. Kaniambia kuwa huyo aliyesimama ni Mzee Said na mkewe (kulia) na katikati ni Shaban Sudi ambae alikuwa mfanyakazi wa bandari na amestaafu kazi mwaka 2015 na kulia kwake ni binti yake. Hapo ilipokuwa nyumba hii hivi sasa kuna ofisi ya CCM. Mimi na Juma sote tulipozaliwa hatukuikuta nyumba hii iliyokuwa Mtaa wa Aggrey. Jirani ya nyumba hii sisi tumekuta nyumba bora zaidi ya Mzee Maleta, nyumba ya Mzee Kleist na nyumba nyingine zilizokuwa katika hali nzuri kupita hii. Nyumba ya Mzee Khube ilikuwa hapo Aggrey na ilikuwa nyumba nzuri. Nyumba hii hivi sasa ni gorofa ndefu na inakabiliana na Msikiti wa Kiblatein moja ya misikiti maarufu ya Dar es Salaam. Waasisi wawili wa TANU Abdulwahid Sykes na Tewa Said Tewa walikuwa wanaishi mtaa huo majirani na si mbali na nyumba hii. Jirani na nyumba hii kwenye kona ya Mtaa wa Aggrey na Sikukuu sisi tulipozaliwa tulikuta jengo zuri la fahari kwa nyakati zile ambalo baadae ikajakuwa ofisi ya Tanganyika Federation of Labour (TFL). Ikitazamana na nyumba hii kwa pembeni kidogo ilikuwa nyumba ya mmoja wa bibi zangu Bi. Debora. Hii nyumba ipo hadi leo lakini imejengwa upya.
Mtaa wa Aggrey kama ulivyo hivi sasa angalia ghorofa zinazojengwa Kariakoo
Picha imepigwa 2014
Posted 11 minutes ago by Mohamed Said
Labels: makala