Huko kwa kuchokana ni kwingine kabisa kwasababu mtu anajua kabisa kachokwa ila hataki kuukubali ukweli.Nnaowaongelea mimi ni wale wazembe wasiojua kujikagua na kuona makosa yao matokeo yake kesi kwa wazee wa dini kila kukicha.
Baby Gal
Umeandika vizuri sana thread yako. Kesi kwenye ndoa za kwenda kwa wazee au viongozi wa dini huwa hazikwepeki. Wee ngoja uolewe halafu utajua ninachosema. Ngoja nikupe stori moja ya jamaa aliyepelekwa kwa wazee kwa kesi ya ndoa. Wazee walishikwa na mshangao kumetokea nini ilhali hawajawahi kusikia mgogoro wowote wa ndoa na mkewe.
Yule jamaa alikuwa na sifa mbili,moja alikuwa mvutaji sana wa sigara(chain smoker) na pili kitandani alikuwa mzima(lijari). Basi kesi ikaanza kusikilizwa kwa mke kuulizwa kulikoni. Mke alisema yafuatayo: ''Mie sina taatizo na mme wangu ila kunajambo linanisumbua sana. Tatizo ni kwamba kama mnavyoona anavuta sigara zake mfululizo(chain smoker) na kitandani akianza ni hivo hovo hakuna kupumzika! Mimi nimeshindwa naona nirudi nyumbani.!''
Huku jamaa akiendelea kupuliza fegi zake mfululizo aliulizwa na wazee kama hayo maneno ni ya kweli. Jamaa alisema ni kweli na akajitetea kuwa amezaliwa hivo hawezi kujizuia. Ndoa ikavunjika. Je, Baby Gal ungelifanyaje kama wewe ndiye ungelikuwa yule mke? Je, ungehimili mapigoya mfululizo au na wewe ungelimpeleka mme kwa wazee?
Kuna kina mama hawana pomzi kwenye tendo la ndoa kama huyu niliyemwelea hapo juu. Matokeo yake ni adiha ndoa kuvunjika au mwanamme kutafuta nyumba ndogo ili awe anamalizia mapigo yake kule.
Lakini pia kuna namna ya kufanya tendo la ndoa kati ya mme na mke. Hilinalo linachangia ndoa nyingi sana kuvunjika au kuwa na nyumba ndogo kwa pande zote mbili. Kuna wanawake hawajui kabisa kuwaridhisha waume zao kwa maana ya kukosa technique za kufanya tendo hilo. Wengine wanasema kifo cha mende au kusoma gazeti. Pia kuna wanaume nao mambo hawawezi kwa maana ya kum-drive mke mpaka anafikia kileleni. Hapa ndipo kwenye matatizo. Nakumbuka kuna madaktari walifanya utafiti kuhusu tendo la ndoa kwa kuongea na wake/waume na wakagundua kuwa kuna wanawake walishakaa kwenye ndoa more than 20 years hawajawahi kufikia kileleni! Mwanamke akiambiwa kupanda kileleni anashangaa ni kitu gani. Sasa siku akionja nje na kufikishwa kwenye hiyo peak basi ndoa itakuwa kwenye hatihati.
Hali kadhalika wanaume.Wakti mwingine wanawake wanachangia mme kutofurahia tendo la ndoa kwa kukosa ubunifu wa kumfanya mme asitoke nje. Kama nim kifo cha mende au kusoma gazeti usitegemee mzee atafurahia tendo hilo. Kwa hiyo siku akionjeshwa nje na wale kina mama wataalamu basi ujue imekula kwako.
Baby Gal ziko changamoto nyingi kwenye ndoa zinazosumbua na kupelekea baadhi ya ndoa kuvunjika. Kwa hiyo get prepared utakapoingia kweny ulingo huo wa ndoa.
Kila lakheri.