Nyumba nzima yateketea kwa moto Kyela. Hakukuwa na msaada wa zimamoto hakuna kilichookolewa

Nyumba nzima yateketea kwa moto Kyela. Hakukuwa na msaada wa zimamoto hakuna kilichookolewa

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Ndivyo hali ilivyotokea mchana wa leo hapa kyela.


Ni mtaa wa Mageleza karibu na chuo cha KPC. Kyela inagari la zimamoto pamoja na wataalamu wa uokoaji.


Chanzo cha moto huo na madhara bado havijajulikana
 
Umejinyima weeee, ukajichanga weee, ukajenga kakibanda kako kwa tabu mara paaap!! Nyiee pole yake mwenye nyumba kwakweli🙆
 
Ndivyo hali ilivyotokea mchana wa leo hapa kyela.View attachment 2676505

Ni mtaa wa Mageleza karibu na chuo cha KPC. Kyela inagari la zimamoto pamoja na wataalamu wa uokoaji.View attachment 2676506

Chanzo cha moto huo na madhara bado havijajulikana
Poleni sana wahanga. Pamoja na yote, mna nafasi ya kufidiwa na TANESCO kama chanzo cha moto kimetokana na mfumo wa umeme. Najua wiring ya ndani haiwahusu TANESCO, ninachotaka kusema ni kuwa msiishie hapo kuona yashatokea basi ndio imeisha. Tulieni, zimamoto watoe taarifa ya chanzo cha moto na ripoti ikitoka mnitafute kwa 0713368153 tushauriane njia ya kwenda. Kama ni fidia, tudai, kama nyumba haikua na umeme basi acha polisi wapambane nayo.
 
Fukuza kazi zimamoto kwa kutozima moto, najua watakuja na sababu lakini hizo sababu ndiyo mwisho wa kazi zao. Labda kwa kifupi ni kwamba, kazi ya zimamoto hakuna tofauti na JWTZ, moto ndiyo adui yako. Ndiyo maana nasema futa kazi hao inawezekana wamevamia taaluma za watu.
1. Gari ya zimamoto iko tayari muda wote.
2. Maji ya kutosha
3. Vifaa vyote vinafanya kazi
4. Gari zaidi ya moja ili muda wote gari ipo tayari.
5. Madereva zaidi ya mmoja
6. Mafuta full muda wote
Fukuza kazi mkuu wao kwa Uzembe siyo Kyela hii.
 
Na nyumba iko sehemu yenye uwazi wa kutosha, mana wangeshatoa kisingizio kua njia haipitiki..

Futuhi kuna mambo ya Ajabu,
Nakumbuka Mwaka 2019 maeneo ya coco beach kuna gari ya zimamoto imefika sehemu ya tukio eti likaanguka maji ya kamwagika, wananchi wakaanza kuzima moto kwa ndoo.
 
Endelea kupambania matumbo ya wachaga wa moshi malafyale wewe
 
Back
Top Bottom