mwez July 2023 nimejenga nyumba ya shambani lkn kipande 1/3 ya nyumba nzima. Ina vyumba 2 vya 3.5x4m na choo. Ina ukubwa wa 8.5x4m imekula bati 27 za futi 10. King post 2m, msumari bati 7kg, msumari 4" 8kg, mbao 2x4 pcs 36 na 2x3 pcs 27. Ikikamilika hii nyumba itakua naukubwa wa 8.5x13m sawa na 110.5sqm. Ushauri wangu kwako kua na picha kubwa kichwani kwako ya nyumba unayotaka alaf jenga vipande vipande. usijenge kama banda au fremu ya duka.
Picha 1: upande wa kushoto.
picha 2: upande wa kulia ntakuendeleza Mungu akipenda. Hapo kwenye tofali chini litakua sebule na open kitchen ya 5x8.5m alaf kitafata kipande kingine kama hii niliyojenga tayari
Picha 3: upande huo wa dirisha moja ni mbele kutaendelezwa kuelekea kulia
Picha 4: nyuma kutaendelezwa kuelekea kushoto
Hii nyumba hapo ilipo mtu unaweza kuishi kigumu
Na amini utakua umepata kitu.