House4Rent Nyumba ya kisasa inapangishwa Kwa Mbonde, Kibaha

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Nyumba ina vyumba vitatu vya kulala (kimoja ni 'master'), jiko, dining place iliyoungana na living room, pamoja na choo cha umma.

Ina ukuta na geti zuri. Fimbo za kisasa za mapazia utazikuta pamoja na waya wa antena/dish.

Pia kuna tanki la maji la lita 3000, stoo ya nje na parking ya kutosha. Pavers kila mahali.

Nyumba ipo mita chache kutoka Morogoro Road, karibu na Uwanja wa Sabasaba. Kwa Mbonde ni kituo baada ya Picha ya Ndege (ukielekea Morogoro), ilipo barabara inayokwenda makao makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania)

Barabara ya kufikia nyumba inapitika kirahisi.

Bei ni Tshs 300,000 kwa mwezi, ila mazungumzo yapo. Kuwa huru!

Kwa mawasiliano: +255 763 600 640

Zingatia: Hakuna dalali.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…