Nyumba ya kupanga inahitajika

Rose

Member
Joined
Jul 30, 2007
Posts
5
Reaction score
0
Natafuta nyumba ya kupanga ambayo ipo tayari kwa kuhamia sasa hivi.
iwe na vyumba 2 vya kulala, sitting room, choo/bafu, jiko,maji, umeme,
parking ya gari kuanzia 2, na usalama.
maeneo: chang'ombe, mivinjeni, kinondoni, makumbusho, kijitonyama, survey,
msasani, namanga, mwenge.
bei 200,000 kwa miezi 6, baada ya miezi 3 ntamalizia iliyobakia.

tafadhali piga namba hii : 0715 400 800
 


KWA LOCATION UNAZOTAKA NA TYPE YA NYUMBA YENYE SPACE KAMA HIZO, KWA BEI HIYO UTAANGAIKA SANA ALAFU HATA ULIPAJI WAKO HAUSHAWISHI,

ni maoni tu
 
Pole dada. najua kutafuta nyumba ni ishu. lakini pia kwa 200,000 na specifications uloweka labda mivinjeni au chang'ombe sina uhakika ila kwa maeneo mengine yalobakia sidhani kama utapata, labda iwe pure lucky. kwa maana kwa bei hiyo sana sana unapata chumba na sebule na parkin may be. all the best lakini
 
Hivi bado kuna nyumba ya 200,000.00 ina vyote ulivyosema !
sidhani dada Rose
 
Du kwa bei hiyo dada yangu inabidi baadhi ya location usitegemee kupata. Ikitokea umepata basi jiandae kuitwa kazini (kama mchana) kuokoa vuombo vyako vya ndani au kama usiku utajikuta unaelea kweny maji!!
 

Mivinjeni na Chang'ombe kwanini una uhakika kwa hizo specifications na bei aliyoweka anaweza kupata?. Sidhani, manake Mivinjeni nakumbuka nyumba kama hiyo anayotaka ziko zile zilizokuwa za Bandari zamani, na kweli zina nafasi kubwa nje, lakini kwa hiyo bei hawezi pata. Na ukumbuke Mivinjeni ni karibu sana na katikati ya jiji, hivyo unapokuwa karibu na katikati ya jiji bei pia huongezeka. Hata kwa Chang'ombe bado ni ngumu kupata kwa hiyo bei.
 
Unaweza kupata ila ubadilishe maeneo ya priorities uliyoyawekaa hapo kwenye bango lako dada Rose
 
Kuna moja inapangangishwa,ni kama kaapatiment lakini temboni maeneo ya lady jyde,ni room moja self,livingroom kubwa,jiko ina tiles,juu gypsum maji ni ya wachina,inasehem ya parking nje. bei Tshs 130,000/= kwa mwezi wasiliana na number hii 0767 48 3665.
 

(red) maana yake nini?
 

mshaurini wapi atapata kwahio 200,000 na aongeze kiasi gani kwa specificaion zake,mkimwambia tu hawezi kupata haitamsaidia kitu,inawezekana 200,000 ndio anaanzia,may be anaweza kuafford hadi 300,000
 
bei za nyumba zimepanda sana jamani.
haya wenye kujua msaidieni ndugu yetu rose jamani labda anaweza kufanikiwa.
namshukuru mungu nilijipinda nikajenga maana hizi kodi si mchezo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…