Nyumba ya Sheikh Hussein Juma, Vice President wa United Tanganyika Party (UTP)

Nyumba ya Sheikh Hussein Juma, Vice President wa United Tanganyika Party (UTP)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NYUMBA YA SHEIKH HUSSEIN JUMA VICE PRESIDENT WA UNITED TANGANYIKA PARTY (UTP)

Rafiki yangu mmoja kaniletea maelezo hayo hapo chini kuhusu picha ya Mtaa wa Mafia na Nyamwezi:

''BRO, HIYO NYUMBA KULIA YENYE MTI, KABLA YA HIYO PEUGEOT NI YA UNCLE WANGU NA MIE NIMEISHI HUMO . NI YA SHEIKH HUSSEIN JUMA KARANDA WA CHAMA CHA UTP.( UNITED TANGANYIKA PARTY).''

Sheikh Hussein Juma alikuwa kati ya masheikh wakubwa Dar es Salaam yeye pamoja na pacha mwenzake Sheikh Hassan Juma.

Hawa ndugu wawili wana historia kubwa katika mji wa Dar es Salaam ya 1950s.

Sheikh Hussein Juma alikuwa kiongozi wa Batetera Union chama cha Wamanyema.

Lakini Sheikh Hussein Juma alifahamika zaidi kwa kuwa Vice President wa United Tanganyika Party (UTP) chama kilichoasisiwa na Wazungu mwaka wa.1955 kuipinga TANU.

Ofisi ya UTP haikuwa mbali na nyumbani kwa Sheikh Hussein Juma.

Ofisi hii ilikuwa Mtaa wa Mafia ukivuka Barabara ya Msimbazi.

Sheikh Hassan Juma yeye alikuwa na shule ikiitwa Al Hasanain Muslim School iliyokuwa Mtaa wa Msimbazi.

Shule hii ikisomesha masomo ya kisekula na Qur'an.

Shule ilifungwa baada ya wazazi kuwatoa watoto wao kwenye shule hiyo kwa kukasirishwa na kitendo cha Sheikh Hussein Juma kujiunga na UTP.

Picha: Sheikh Hussein Juma aliyevaa kofia nyeupe, Mtaa wa Mafia na Nyamwezi na kulia ni Sheikh Hussein Juma na kushoto Sheikh Hassan Juma.

1656264413331.png
1656264447436.png
1656264471488.png
 
Back
Top Bottom